Posts

BILLICANAS YA MBOWE YAANZA KUBOMOLEWA RASMI

Image
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limeanza kubomoa jengo la iliyokuwa Klabu Bilicanas na ofisi za Free Media inayomiliki gazeti la Tanzania Daima zinazomilikiwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe, lililopo makutano ya barabara ya Mkwepu na Indira Gandhi lenye kitalu namba 725-726/24 na hati namba C. T No. 186018/15 and C. T No. 186018/10. Ubomoaji huo ulioanza jana unafanyika wakati Mbowe ameingia katika mgogoro na NHC baada ya kampuni ya udalali ya Poster and General Traders kumtolea vyombo nje mwanzoni mwa Septemba, mwaka jana kwa kudaiwa Sh bilioni 1.2 ambayo ni deni la pango ya miaka 20. Mwanzoni mwa Septemba, mwaka jana NHC kwa kushirikiana na Kampuni ya Poster and General Traders, ilifika katika jengo hilo kwa maelekezo ya kutoa thamani mbalimbali zilizokuwa katika ofisi za jengo hilo na kumpa Mbowe siku 14 kulipa deni analodaiwa na kuweza kugomboa mali hizo. Mpango huo ulisimamiwa na Meneja

MAJALIWA ACHARUKA,KUMTUMA CAG KUKAGUA TANCOAL

Image
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa atamtuma mara moja Msajili wa Hazina, aende kufanya uchunguzi wa kina na wa kijinai (forensic investigation) ili kijiridhisha kama mapato na matumizi ya kampuni ya TANCOAL ni halali.Alitoa kauli hiyo jana mara baada ya kupokea taarifa na kutembelea mgodi huo ili kuona shughuli za uzalishaji zikoje.Waziri Mkuu alisema atamuagiza pia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ya Serikali (CAG) ili apitie mahesabu ya kampuni hiyo tangu mwaka 2011 walipoanza uzalishaji. “Mbali na CAG, itabidi Gavana wa Benki Kuu naye aangalie utumaji wa fedha uliokuwa ukifanywa kama ulifanyika kwa halali,” alisema. Katika maswali aliyoyauliza Waziri Mkuu, alitaka kufahamu ni kwa nini kampuni hiyo haijalipa gawio kwa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) ambao ni mbia (asilimia 30) na kampuni ya Intra Energy Limited (asilimia 70), licha ya kuwa imekuwa ikifanya uzalishaji wa makaa ya mawe na kuyasafirisha kwenye viwanda hapa nchini na nje ya nchi. “Taarifa

HUMPHREY POLEPOLE ATOA MSIMAMO WAKEKUHUSU KATIBA MPYA

Image
Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambaye kwa sasa ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole ameweka wazi msimamo wake kuhusu mchakato wa katiba mpya, na kusema kuwa hajalitelekeza suala hilo. Humphrey Polepole akiwa Kikaangoni Polepole aliyekuwa kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV kupitia facebook.com/eatv.tv, katika mahojiano yake na East Africa Radio amesema kuwa mchakato wa kuipata katiba mpya kwa Tanzania uko kwenye mikono salama chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, na kuwataka watanzania waiache serikali irekebishe kwanza baadhi ya mambo ili mchakato huo utakapoanza usikumbwe na vikwazo. Polepole amesema kwa uzoefu wake kama mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba, anafahamu mambo ambayo watanzania waliyataka na kwamba mambo hayo ndiyo ambayo yameanza kutekelezwa na serikali ya awamu ya tano ikiwemo kuwa kujali utu, kudhibi

Gigy Money Afunguka Suala la Kuwa Ana Ukimwi, Orodha ya Wanaodaiwa Kutoka Naye Yatajwa

Image
Video queen matata ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha redio moja jijini hapa, Gift Stanford ‘Gigy Money’, ametema cheche akisema kuwa, watu wote wanaomsema kwamba kutokana na kuvaa nusu utupu na kujiachia na midume mbalimbali huenda ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi, waache kwani kama ni kweli basi wengi wangekufa kwa sababu ameshatembea na mastaa kibao Bongo. Gigy Money Akizungumza na gazeti hili juzi, Gigy alisema kwamba amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mastaa mbalimbali wakubwa Bongo akiwemo Mbongo Fleva, Ali Kiba na kudai kuwa, kama kuambukizwa virusi angeanza yeye na wengine wangefuata. “Unajua watu wanashangaza sana. Kama mtu ana virusi vya Ukimwi hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu anayempenda, ningependa watu waache unyanyapaa. Ninachojua mimi sina Ukimwi kwa kuwa nilipima kwa shinikizo la mpenzi wangu wa sasa (Moulad Alpha ‘Moj’) na watu niliotembea nao wanaendelea vizuri tu, wengine wachumba zao wananyonyesha,” alisema Gigy.

Hali si Shwari Wolper na Harmonize….Meseji Aliyopost Wolper Yaonyesha Wameachana

Image
Jacline Wolper ame post hii halaf ghafla kafuta, hii maana yake nini wadau? Jisomee alichoandika kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram:

WAZIRI MKUU AIPONGEZA BIMA YA AFYA KWAJINSI INAVYO SAIDIA KUTOA HUDUMA KATIKA KITUO CHA AFYA CHA MADABA SONGEA

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimjulia hali Sophia Mgeni ambaye ametoka kujifungua mtoto wa kike, Waziri mkuu alitembelea Zahanati ya Madaba iliyopo wilaya ya Songea ili kuwasikiliza wagonjwa katika zahanati hiyo Waziri mkuu yupo Mkoani Ruvuma kwa ziara ya kukagua shughuli za maendeleo  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wauguzi wa zahanati ya Madaba huku akiwataka waendelee na moyo waliokuwa nao wa kuwapenda wagonjwa na kuwahudumia, kwani serekali inatambua mchango wao wanaoutoa kwa taifa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi wa madaba waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza,Waziri Mkuu alitumia nafasi hiyo kuwaelezaa Wananchi hao juhudi za serekali za kuwasaidia katika sekta mbali mbali ikiwemo Huduma ya bima ya afya. Waziri mkuu yupo mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi.Picha na Chris Mfinanga

CLINTON KUSHUHUDIA DONALD TRUMP AKIAPISHWA MAREKANI

Image
Hillary Clinton na mumewe Bill wamethibitisha kwamba watahudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais mpya wa Marekani Donald Trump mjini Washington DC. George W Bush na mkewe Laura pia wametangaza kwamba wanapanga kuhudhuria sherehe hiyo mnamo tarehe 20 Januari. Wamesema wanataka "kushuhudia kukabidhiwa madaraka kwa rasi mwingine kwa njia ya amani." Tajiri huyo kutoka Manhattan, New York ataapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani katika makao makuu ya serikali Capitol Hill. Bw Trump alimshinda Bi Clinton katika uchaguzi mkuu uliofanyika Novemba mwaka jana na amemkosoa Bw Bush kutokana na vita vya Iraq na mashambulio ya 9/11. Kabla ya tangazo hilo la Jumanne, Jimmy Carter alikuwa ndiye rais wa zamani pekee aliyekuwa amesema angehudhuria sherehe hiyo. Rais mwingine mstaafu George HW Bush, 92, amesema hataweza kuhudhuria kutokana na umri wake. Bi Clinton amekuwa haonekani sana hadharani tangu aliposhindwa na Bw Trump uchaguzini Novemba. Wakati wa kampeni, Bw

Mwanamke wa kwanza kugombea urais Tanzania afariki dunia

Image
Mwanamke wa kwanza kugombea urais nchini Tanzania, Dkt. Anna Senkoro amefariki dunia leo ambapo Hospitali ya Taifa Muhimbili imethibitisha kutokea kwa kifo hicho. Dkt. Senkoro ndiye mwanamke wa kwanza kugombea urais nchini Tanzania ambapo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 alipeperusha bendera ya chama za PPT- Maendeleo. Katika uchaguzi huo mgombea wa CCM, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliibuka mshindi. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, PPT- Maendeleo kilimtangaza Dkt. Anna Senkoro kuwa mgombea wake lakini alikihama chama hicho na kijiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo alitimkia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) siku chache kabla ya kampeni kuanza. Mbali na masulaa ya kisiasa, Anna Senkoro alikuwa ni Daktari na pia mama wa watoto watatu

ANASWA AKIFUKUA KABURI LA ALBINO

Image
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kufukua kaburi la marehemu ambaye likuwa ni mlemavu wa ngozi (Albino) aliyefariki mwaka 2010 kwa lengo la kuchukua viungo vyake.Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa na Kamanda a Polisi Mkoani Mbeya DCP Dhahiri Kidavashari inasema kuwa mnamo tarehe 03.01.2017 majira ya saa 01:00 usiku katika Kijiji cha Mumba kilichopo Kata ya Ilembo, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la JONAS JOHN mkazi wa Chapakazi alikamatwa na askari Polisi akiwa na wenzake wawili wakifukua kaburi la marehemu SISTER OSISARA aliyekuwa mlemavu wa ngozi (ALBINO) Inadaiwa kuwa marehemu alifariki dunia mwaka 2010 kwa ugonjwa wa homa na kuzikwa katika makaburi ya Kijiji cha Mumba. Mtuhumiwa alikutwa na majembe na makoleo ambayo walikuwa wakiyatumia kufukuria kaburi hilo. Baada ya mahojiano mtuhumwa huyo aliwataja washirika wenzake wawili ambao walikimbia baada ya kuwaona askari. Jeshi hilo linaendelea na msako mkali wa kuwatafuta watuhu

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI MSIBA WA MZEE MAARUFU WA CHATO ADMIRABILIS MBABE MANYAMA (82) CHATO MKOANI GEITA

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole    Bi Mugwe Mbabe ambaye ni Mke mkubwa wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Bi. Regina Mbabe mke mdogo wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe (82) Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Deodatus Manyama wakwanza (kushoto) ambaye ni mdogo wa marehemu Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Chato mkoani Geita.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Bi. Mugwe Mbabe mke mkubwa wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

SUPERSTAA DIAMOND PLATNUMZ ATOA TOFAUTI HII KUHUSU WATOTO WAKE

Image
Diamond amekuwa ni mmoja kati ya wasanii ambao wanaendesha maisha yao kibiashara, kuthibitisha hilo ni hivi tunavyoona mambo yanayo endelea kwenye familia yake. Kama ni mfatiliaji wa familia ya Bw. Nasib (Diamond) Abdul basi utakuwa tayari ushaona utofuti uliopo baina ya watoto wake wawili, hapa namzungumzia  Princess Tiffah  pamoja na  Prince Nillan. Kipindi mwanae wa kike Tiffah, baada ya kuzaliwa alikuwa ni mtoto ambae kapokea shamra shamra nyingi za hatari kutoka kwenye familia yake na kupata deal kubwa za matangazo katika umri mdogo lakini kwa Nillan ambe ni mdogo wake na Tiffah imekuwa si hivyo tulivyotarajia kuoa tulio wengi. Prince Nillan Je ni kwanini mbwembwe zilizo kuwepo kwa Latifah hazijawa kwa Nillan? Akipiga story na Clouds E! ya Clouds Tv, Diamond alisema  “Wanawake wameumbiwa mashauzi ndio maana Tiffah tumemshauzisha, lile ni dume (Nillan) linawinda, kwanza jina lake kutoka ilikuwa tatizo, tunabishana kila mtu anataka jina lake, mpak

DIAMOND, ALIKIBA, NAVY KENZO NA HARMONIZE WASHINDA WATSUPTV AFRICAN AWARDS 2016.

Image
Huenda mwaka 2016 ukawa unaenda kuisha vizuri kwa  wakilishi wetu kujinyakulia tuzo huko Ghana.Usiku wa December 28 2016 tuzo za  WatsUp TV Africa Music Video Awards 2016  ndio zilitangazwa  Accra Ghana , washindi 22 walitangazwa kupitia  Press Conference  wakiwemo wasanii wa  Tanzania  waliyofanikiwa kushinda tuzo hizo kwa mwaka 2016. Kama hufahamu  WatsUp TV Africa Music Video Awards  (WAMVA) ni tuzo ambazo zinaandaliwa na  WatsUP TV , zikiwa na lengo la kushawishi au kuhamasisha wasanii kufanya video za viwango vya juu pamoja na ubora. Kama hufahamu  WatsUp TV Africa Music Video Awards  (WAMVA) ni tuzo ambazo zinaandaliwa na  WatsUP TV , zikiwa na lengo la kushawishi au kuhamasisha wasanii kufanya video za viwango vya juu pamoja na ubora. Wametangazwa washindi 22 wasanii na waongozaji wa video 170 waliyokuwa wametajwa kuwania tuzo hizo wakati zinazinduliwa mwezi September 2016,  kwa mujibu wa mtandao wa  Zionfelix.net  ni kuwa washindi watafanya show katik

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MKOANI LINDI KWA ZIARA YA KIKAZI KATIKA WILAYA YA RUANGWA

Image
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Lindi Godfrey Zambi mara alipowasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea kwa ajili ya ziara ya kikazi katika wilaya ya Ruangwa Mkoani lindi kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi  Alli Mohamed Mtopa  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkurugenzi wa Nachingwea (DED) Bakari Mohamedi Bakari katika kiwanja cha ndege cha Nachingwea wakati wa mapokezi ya waziri mkuu wilayani hapo waziri mkuu amefika kwa ziara ya kikazi katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi  Waziri mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mery Majaliwa wakifurahia ngoma ya kikosi cha JKT  843KJ kilichopo Nachingwea ambacho kilikuwepo katika mapokezi ya Waziri Mkuu katika uwanja wa ndege wa Nachingwea .Picha na Chris Mfinanga

MWANAFUNZI ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUKATWA MAPANGA NA MWALIMU

Image
MWANAFUNZI Marco Limbe(14) aliyemaliza darasa la saba mwaka huu katika shule ya msingi Yitwimila iliyoko kata ya kiloleli wilaya ya Busega mkoani Simiyu amelazwa katika kituo cha afya Busega mara baada ya kuchalangwa mapanga kichwani na mdomoni na mwalimu wake. Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11.30 jioni wakati mwanafunzi huyo alipokuwa akirejea nyumbani kwao akitokea katika malisho ya mifugo ndipo alipokaribia katika shamba la mwalimu Pendo Gabriel ndipo mwalimu huyo alimkamata kijana huyo na kuanza kumchalanga kwa panga na kupelekea kijana limbe kupoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 mara baada ya kufikishwa katika kituo cha afya Busega. “Shuhuda wa tulio hilo aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Manoga anaeleza kuwa ilikuwa kama mchezo lakini kumbe ni kweli kwani niliona mifugo ya limbe iliyokuwa ikielekea nyumbani na huku limbe akiwa nyuma ya mifugo hiyo katika barabara ambalo liko karibu na maeneo ya shule ghafla nilimuona mwalimu pendo w