CLINTON KUSHUHUDIA DONALD TRUMP AKIAPISHWA MAREKANI

Hillary Clinton na mumewe Bill wamethibitisha kwamba watahudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais mpya wa Marekani Donald Trump mjini Washington DC.
George W Bush na mkewe Laura pia wametangaza kwamba wanapanga kuhudhuria sherehe hiyo mnamo tarehe 20 Januari. Wamesema wanataka "kushuhudia kukabidhiwa madaraka kwa rasi mwingine kwa njia ya amani."
Tajiri huyo kutoka Manhattan, New York ataapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani katika makao makuu ya serikali Capitol Hill. Bw Trump alimshinda Bi Clinton katika uchaguzi mkuu uliofanyika Novemba mwaka jana na amemkosoa Bw Bush kutokana na vita vya Iraq na mashambulio ya 9/11.
Kabla ya tangazo hilo la Jumanne, Jimmy Carter alikuwa ndiye rais wa zamani pekee aliyekuwa amesema angehudhuria sherehe hiyo. Rais mwingine mstaafu George HW Bush, 92, amesema hataweza kuhudhuria kutokana na umri wake.
Bi Clinton amekuwa haonekani sana hadharani tangu aliposhindwa na Bw Trump uchaguzini Novemba. Wakati wa kampeni, Bw Trump alimweleza kama mtu mwovu na asiye wa kuaminika.
Bw Trump pia amekosoa madai ya George W Bush kwamba alihakikisha Wamarekani walikuwa salama zaidi wakati wa utawala wake. Alisema shambulio la Septemba 11 mwaka 2001 (9/11) lilitekelezwa wakati wa utawala wake.Aidha, amemshutumu rais huyo wa 43 kwa kusema uongo kuhusu kuwepo kwa silaha za maangamizi makubwa nchini Iraq. Bw Trump alishambulia pia mtu mwingine wa familia ya Bush, gavana ya Florida Jeb Bush ambaye alikuwa anakabiliana naye kwenye mchujo chama cha Republican na kumtaja kama "aliyepungukiwa na nguvu".


Chanzo: BBC Swahili

Comments

Popular posts from this blog