HUMPHREY POLEPOLE ATOA MSIMAMO WAKEKUHUSU KATIBA MPYA
Aliyekuwa
mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambaye kwa sasa ni Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole ameweka
wazi msimamo wake kuhusu mchakato wa katiba mpya, na kusema kuwa
hajalitelekeza suala hilo.
Humphrey Polepole akiwa Kikaangoni
Polepole
aliyekuwa kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV kupitia
facebook.com/eatv.tv, katika mahojiano yake na East Africa Radio amesema
kuwa mchakato wa kuipata katiba mpya kwa Tanzania uko kwenye mikono
salama chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, na kuwataka watanzania
waiache serikali irekebishe kwanza baadhi ya mambo ili mchakato huo
utakapoanza usikumbwe na vikwazo.
Polepole
amesema kwa uzoefu wake kama mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
iliyokuwa chini ya Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba, anafahamu
mambo ambayo watanzania waliyataka na kwamba mambo hayo ndiyo ambayo
yameanza kutekelezwa na serikali ya awamu ya tano ikiwemo kuwa kujali
utu, kudhibiti rasilimali za umma, kuwataka wabunge wakae majimboni n.k.
Katika
hatua nyingine, Polepole amewataka wanasiasa kwa sasa waache
kuzungumzia suala la Katiba na badala yake wazungumzie ufisadi ili
kuongeza nguvu katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi.
Comments
Post a Comment