Mwanamke wa kwanza kugombea urais Tanzania afariki dunia


rais
Mwanamke wa kwanza kugombea urais nchini Tanzania, Dkt. Anna Senkoro amefariki dunia leo ambapo Hospitali ya Taifa Muhimbili imethibitisha kutokea kwa kifo hicho.
Dkt. Senkoro ndiye mwanamke wa kwanza kugombea urais nchini Tanzania ambapo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 alipeperusha bendera ya chama za PPT- Maendeleo. Katika uchaguzi huo mgombea wa CCM, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliibuka mshindi.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, PPT- Maendeleo kilimtangaza Dkt. Anna Senkoro kuwa mgombea wake lakini alikihama chama hicho na kijiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo alitimkia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) siku chache kabla ya kampeni kuanza.
Mbali na masulaa ya kisiasa, Anna Senkoro alikuwa ni Daktari na pia mama wa watoto watatu

Comments

Popular posts from this blog