Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu kwa jina la Mzee wa Upako jana amesema waandishi wote wa habari wanaoandika habari za kumchafua, watakufa kabla ya kufika Machi 2017. Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake na kulewa. āKila mwandishi aliyeniandika vibaya, ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu ndiye ataamua kwamba ama niache kuhubiri mimi au wewe ufe ā¦najua hata leo mko humu mmekuja na mnasikiliza tu,ā alisema. āAkisema Mungu uishi wewe basi, nakuwa sina namna, lakini sijawahi kumtumikia Mungu ambaye ananyamaza. Nilishakubaliana mimi na Mungu, mpango wa Mungu ndiyo mpango wangu, sasa wajiandae, mimi siyo Sheikh Yahaya, mmeingia choo cha kike, nasema āMama yangu mzaziā nitaacha kuhubiri, nitaacha kuhubiri ā¦.mimi ...