Posts

Rais JPM Awaongoza Mamia Kuagwa Mwili wa Samuel Sitta Karimjee Dar

Image
Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Spika wa Bunge Mstaafu, Samuel John Sitta. …Akiwapa mkono wa pole wafiwa wa marehemu Sitta baada ya kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza. Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete akipita mbele ya jeneza kutoa heshima zake za mwisho. Makamu wa Rais Mstaafu, Dk. Gharib Bilal akipita mbele ya jeneza kuuaga mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge Mstaafu, Samwel Sitta. Viongozi mbalimbali wakiwa msibani hapo. Mbunge wa Muleba Kusini, Prof. Anna Tibaijuka (katikati) akiwa na waombolezaji wengine katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. …Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi naye akipita mbele kuuaga mwili wa marehemu Sitta. Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye akipita mbele ya jeneza kuuaga mwili wa marehemu. Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba naye akipita mbele ya jeneza kutoa heshima za mwisho.

Obama: ‘Ninamuunga Mkono’ Donald Trump, Nitashirikiana Naye

Image
MAREKANI: Rais mteule wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa ni ”heshima” kubwa kukutana na rais Barrack Obama katika mazungumzo ya mpito yaliofanyika katika ikulu ya White House. Rais Obama amesema kuwa ametiwa moyo kuhusu mazungumzo yao ya maswala mbalimbali yaliochukua zaidi ya saa moja. Trump ametilia shaka uraia wa rais Obama na kuapa kuharibu ufanisi wake wakati wa utawala wake. Bw Trump kwenye kampeni alimweleza Bw Obama kama rais mbaya zaidi kuwahi kuongoza Marekani. Wakati wa kampeni bwana Obama alisema kuwa bwana Trump ‘hafai’ kuongoza Marekani. Pia alisema Mwanarepublican huyo hana sifa na uwezo wa kuwa kiongozi wa Marekani. Mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York, ambaye sasa ni rais mteule, kwa muda mrefu alitilia shaka uhalali wa habari kwamba Obama alizaliwa Hawaii, na alikejeliwa hadharani na Rais Obama. Wawili hao walishauriana kwa zaidi ya saa moja afisi ya rais katika ikulu ya White House mnamo Alhamisi na walipojitokeza kwa wanahaba

Tanzia: Mbunge Hafidh Ali Tahir Afariki Dunia

Image
DODOMA: Mbunge wa Jimbo la Dimani lililopo visiwani Zanzibar, Mhe. Hafidh Ali Tahir (CCM) amefariki dunia saa 9 alfajiri ya leo katika Hospitali ya General iliyopo mkoani Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu. Marehemu alizaliwa Oktoba 30, 1953 na aliwahi kuwa Mkuu wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (1970-1978) na amekuwa mbunge tangu 2005 hadi mauti yanamkuta. Marehemu pia alikuwa mwanamichezo, mwamuzi wa FIFA na mpenzi wa Klabu ya Yanga kindakindaki na ni jana tu alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Tawi la wabunge Wana-Yanga mjini Dodoma chini ya Uenyekiti wa Venance Mwamoto. Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitatolewa hapo baadae. Mhe. Spika anaungana na Wabunge wote katika kuomboleza msiba huu.

Mwili wa Samuel Sitta Ulivyopokelewa Uwanja wa Ndege Dar

Image
Mwili  wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta umewasili jioni hii katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ukitokea nchini  Ujerumani ambako alikuwa akitibiwa hadi mauti yalipomfika.  Mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege mwili wa Marehemu Sitta utapelekwa nyumbani kwake Msasani, Dar es Salaam.

RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA WAGONJWA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

Image
 Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimjulia hali mke wake, Mama Janeth Magufuli, ambaye amelazwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu leo Novemba 10, 2016  Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimjulia hali mke wake, Mama Janeth Magufuli, ambaye amelazwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu leo Novemba 10, 2016.  : Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimjulia hali Waziri wa Zamani Balozi Ramadhani Mapuri ambaye amelazwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu leo Novemba 10, 2016.   Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru na kuwapongeza kwa kazi nzuri baadhi ya madaktari na wauguzi kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Tai

Rais Magufuli Amlilia Mungai

Image
RAIS wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John  Pombe Magufuli leo amemlilia aliyewahi kuwa waziri katika awamu zote nne za uongozi nchini, Marehemu Joseph Mungai ambaye mwili wake umeagwa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Rais Magufuli akiwaongoza Watanzania katika kuuaga mwili wa Mungai, alishindwa kuficha hisia zake wakati wa kuaga mwili wa marehemu na kutokwa na machozi, jambo lililopelekea kutoa kitambaa cha mkononi na kujifuta. Mbali na rais,  wengine walioshindwa kujizuia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Lawrence Masha na viongozi wengine. Viongozi wengine waliofika kuuaga mwili wa Mungai ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa, Makamu wa Rais Mstaafu, Dk. Ghalib Bilal, Mama Salma Kikwete, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Daniel Lubuva, Jaji Joseph Warioba, Mzee Kingunge, Mzee John Cheyo, Steven Wassira, Spik