Obama: ‘Ninamuunga Mkono’ Donald Trump, Nitashirikiana Naye
MAREKANI: Rais mteule wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa ni ”heshima” kubwa kukutana na rais Barrack Obama katika mazungumzo ya mpito yaliofanyika katika ikulu ya White House.
Rais Obama amesema kuwa ametiwa moyo kuhusu mazungumzo yao ya maswala mbalimbali yaliochukua zaidi ya saa moja.
Trump ametilia shaka uraia wa rais Obama na kuapa kuharibu ufanisi wake wakati wa utawala wake.
Wakati wa kampeni bwana Obama alisema
kuwa bwana Trump ‘hafai’ kuongoza Marekani. Pia alisema Mwanarepublican
huyo hana sifa na uwezo wa kuwa kiongozi wa Marekani.
Mfanyabiashara
huyo tajiri kutoka New York, ambaye sasa ni rais mteule, kwa muda mrefu
alitilia shaka uhalali wa habari kwamba Obama alizaliwa Hawaii, na
alikejeliwa hadharani na Rais Obama.
Wawili
hao walishauriana kwa zaidi ya saa moja afisi ya rais katika ikulu ya
White House mnamo Alhamisi na walipojitokeza kwa wanahabari, walijaribu
kuficha uadui kati yao.
Hata hivyo Obama alisema kuwa ”anamuunga” mkono baada ya kumshinda Hillary Clinton.
Baada
ya mkutano huo wa Ikulu rais Obama alisema kuwa kipaombele chake sasa
katika miezi miwili ijayo ni kuhakikisha kuwa kundi litakalosimamia
shughuli za mpito linafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Alisema
kuwa wamezungumza sera za nyumbani pamoja na zile za kigeni na kwamba
amefurahishwa na maoni ya Donald Trump kwamba yuko tayari kufanya kazi
na rais Obama katika maswala yanayokabili Marekani.
Bwana Trump amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na rais Obama katika siku zijazo.
Comments
Post a Comment