Rais JPM Awaongoza Mamia Kuagwa Mwili wa Samuel Sitta Karimjee Dar
Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Spika wa Bunge Mstaafu, Samuel John Sitta.
…Akiwapa mkono wa pole wafiwa wa marehemu Sitta baada ya kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete akipita mbele ya jeneza kutoa heshima zake za mwisho.
Makamu wa Rais Mstaafu, Dk. Gharib Bilal akipita mbele ya jeneza kuuaga mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge Mstaafu, Samwel Sitta.
Viongozi mbalimbali wakiwa msibani hapo.
Mbunge wa Muleba Kusini, Prof. Anna Tibaijuka (katikati) akiwa na waombolezaji wengine katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
…Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi naye akipita mbele kuuaga mwili wa marehemu Sitta.
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye akipita mbele ya jeneza kuuaga mwili wa marehemu.
Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba naye akipita mbele ya jeneza kutoa heshima za mwisho.
Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo akimpa mkono wa pole mtoto wa marehemu aitwaye, Benjamin Sitta.
Waombolezaji wakiongozwa na aliyekuwa Waziri wa Fedha wa zamani, Basil Mramba, wakipita mbele ya wafiwa kutoa mkono wa pole.
Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim Lipumba akiwapa mkono wa pole wafiwa baada ya kutoa heshima zake za mwisho mbele ya jeneza.
Viongozi mbalimbali wakipita mbele ya jeneza kutoa heshima zao za mwisho.
Waombolezaji wakipita mbele kutoa heshima zao za mwisho.
Watu wakiwa kwenye mstari kutoa heshima zao za mwisho.
Ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu wakiwa na simanzi msibani hapo.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli leo ameongoza mamia ya waombolezaji wa
Jiji la Dar es Salaam wakiwemo viongozi wa serikali na vyama mbalimbali
kuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Samuel Sitta. Zoezi hilo limefanyika katika Viwanja vya
Karimjee jijini Dar es Salaam.
Viongozi wengine waliofika kuuaga mwili
wa Sitta ni pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete,
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa, Makamu wa Rais
Mstaafu Dk. Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye, Waziri
Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi
John Kijazi, Mbunge wa Muleba Kusini, Prof. Anna Tibaijuka, Mwenyekiti
wa Chama cha UDP John Cheyo, Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili
wa Vyama vya Siasa Prof. Ibrahim Lipumba na wengine wengi.
Baada ya zoezi la kuaga, mwili wa Sitta
umesafirishwa kwenda mkoani Dodoma ambako utaagwa na wabunge wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kisha kusafirishwa kwenda Urambo mkoani
Tabora kwa mazishi yatakayofanyika kesho Jumamosi.
Marehemu Sitta alifariki dunia
Novemba 07 mwaka huu katika Hospitali ya Technal University iliyopo
nchini Ujerumani alipokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya saratani ya
tezi dume.
MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI. AMENPICHA NA DENIS MTIMA/GPL
Comments
Post a Comment