Rais Magufuli Amlilia Mungai



jpm-newdk-ghalib-bilal-akiaga dsc_0228 jaji-warioba-akitoa-heshima jeneza-la-mungai kushoto-ni-kaka-wa-marehemu lukuvi mama-salma-kikwete-akimfari mkurugenzi-wa-global-publis mzee-kingunge-akisalimia-na mzee-mkapa-akisalimia-na-mk mzee-mkapa-na-sumaye-wakiwa picha-ya-marehemu-mungai-en rais-john-pombe-magufuli-ak shigongo-akipita-mbele-ya-j waziri-mahiga-akizungumza waziri-mstaafu-fredrick-su
RAIS wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John  Pombe Magufuli leo amemlilia aliyewahi kuwa waziri katika awamu zote nne za uongozi nchini, Marehemu Joseph Mungai ambaye mwili wake umeagwa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli akiwaongoza Watanzania katika kuuaga mwili wa Mungai, alishindwa kuficha hisia zake wakati wa kuaga mwili wa marehemu na kutokwa na machozi, jambo lililopelekea kutoa kitambaa cha mkononi na kujifuta.
Mbali na rais,  wengine walioshindwa kujizuia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Lawrence Masha na viongozi wengine.
Viongozi wengine waliofika kuuaga mwili wa Mungai ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa, Makamu wa Rais Mstaafu, Dk. Ghalib Bilal, Mama Salma Kikwete, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Daniel Lubuva, Jaji Joseph Warioba, Mzee Kingunge, Mzee John Cheyo, Steven Wassira, Spika wa Bunge Mstaafu,  Pius Msekwa na wengine.
Mwili wa marehemu utasafirishwa kesho kuelekea Mafinga, mkoani Iringa kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Jumamosi.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE!
Picha / Habari: Denis Mtima, Gabriel Ng’osha/GPL

Comments

Popular posts from this blog