Posts

RC Makonda Azindua Chama Cha Waendesha Bodaboda Na Bajaj Mkoa Wa Dar es Saalam

Image
Mkuu wa mkoa Paul Makonda akihutubia. Sehemu ya umati ya waendesha bodaboda waliojitokeza. Mmoja wa madereva aliyeshiriki zoezi hilo akiwa kwenye muonekano mpya. Mkuu wa Mkoa akiongozana na baadhi ya viongozi wa chama hicho. Sehemu ya umati waliohudhuria zoezi hilo. Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akivaa koti kama ishara kwa madereva wote ambao watapaswa kuvaa wawapo safarini. Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akijianda kuvaa Helmet. Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akiwa tayari kuvaa kofia nguvu ‘Helmet.’ Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akiwa katika muonekano mpya wa madereva wa bodaboda. Mkuu wa Mkoa akiongoza maandamano ya waendesha bodaboda yaliyoanzia viwanja vya Biafra na kuishia viwanja wa Leaders, Kinondoni. Kopro Rioba akieleza jambo kwenye uzinduzi huo. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mheshimiwa Paul Makonda, mapema leo amezindua Chama cha Waendesha Bodaboda na Bajaj kwa Mkoa wa Dar es Salaam. Pia ameongoza maandamano ya waendesha bodaboda kuanzia viwanja vya Biafra hadi viwanja vya Leade

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA, AKABIDHIWA MSAADA WA DOLA LAKI MBILI UTOKA KWA RAIS MUSEVENI WA UGANDA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi mchango wa fedha cha dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) - takriban Tshs. 437,000,000/- taslimu uliotolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kusaidia waathirika watetemeko la ardhi mkoani Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea msaada wa fedha cha dola laki mbili za Kimarekani (USD 200,000) -takriban Tshs. 437,000,000/- taslimu kutoka kwa Balozi wa Uganda hapa nchini Mhe. Doroth Samali Hyuha ( wa pili kutoka kushoto) akiwa pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Elibariki Maleko. Msaada huo umetolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa Tetemeko la ardhi mkoani Kagera leo Ikulu jijini Dar es salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Rais wa

MKUU WA WILAYA YA ILALA AONGOZA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUCHANGIA MAAFA YA TETEMEKO BUKOBA

Image
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akipokea kiasi cha shilingi milioni zaidi ya milioni 6 kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara wa Kariakoo Bw. Deo Senya wakati Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK) walipofanya Harambee ya kuchangia wahanga wa Tetemeko la Ardhi kule Bukoba mkoani Kagera ambapo Mkuu wa wilaya hiyo aliongoza harambee hiyo, Kuliani ni Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala Bw. Edward Mpogolo na katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanya Biashara Kariakoo Bw.Philimin Lomano Chonde. Katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 13,708,000/= fedha taslimu zilikusanywa na vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 31564800/= jumla ya michango kwa ujumla ni shilingi milioni 45,672,800/= harambee hiyo leo ilikuwa inazinduliwa rasmi na michango inaendelea mpaka siku ya jumamosi ijayo ambapo ndiyo harambee hiyo itafungwa rasmi na wafanyabiashara mbalimbali wametakiwakuendelea kuchangia kwa kupitia jumuiya yao ya wafanyabiashara mpaka

Zombe na Wenzake Washinda Kesi, Christopher Bageni Kunyongwa

Image
Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kinondoni,  SP Christopher Bageni (kushoto) baada ya kuhukumiwa kunyongwa akiagana na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi,  (ACP) Abdallah Zombe (katikati). …Akiongea jambo na aliyekuwa wakili wake baada ya hukumu kutolewa. Polisi wakimpeleka katika chumba maalum mahakamani  baada ya hukumu kutolewa. Bageni akielekea katika chumba maalum. Abdallah Zombe (mwenye nguo nyeupe katikati) akiwa na ndugu zake baada ya kuachiwa huru.  BAADA  ya kimya kirefu, Mahakama ya Rufaa leo imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi,  (ACP) Abdallah Zombe, na maofisa wenzake wawili. Hata hivyo, mahakama hiyo imemuhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kinondoni,  SP Christopher Bageni. Zombe na wenzake walikuwa wakituhumiwa kuwaua wafanyabiashara watatu wa Mahenge Morogoro na teksi dereva mmoja

Jacqueline Mengi Afanya Uzinduzi Wa Duka La Samani (Molocaho – Amorette)

Image
Mrembo wa taji la Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na wageni walikwa pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa duka lake la samani za ndani “Amorette” lililopo katika jengo la Village Walk gorofa ya kwanza karibu na Sea Cliff Hotel, Masaki jijini Dar es Salaam. Muonekano wa nje utaokutambulisha hili ndio duka la “Amorette”  Bi. Jacqueline Mengi akikata utepe kuzindua duka lake hilo. Ha ha ha ha, sasa mko huru kuingia wageni waalikwa kujionea yaliyomo,…..Bi. Jacqueline Mengi akifurahi jambo mara baada ya kukata utepe. Bi. Jacqueline Mengi akiongozana na baadhi ya wageni waalikwa kuingia ndani ya duka la “Amorette” Balozi Juma Mwapachu na baadhi ya wageni waalikwa wakiangalia moja ya meza ya chakula (dining table) iliyotengenezwa kwa mbao aina ya Mninga baada ya kuzinduliwa duka hilo lililopo katika jengo la Village Walk, Masaki jijini Dar. Wageni waalikwa wakiendelea kukagua samani mbalimbali katika duka