RC Makonda Azindua Chama Cha Waendesha Bodaboda Na Bajaj Mkoa Wa Dar es Saalam
Mkuu wa mkoa Paul Makonda akihutubia.Sehemu ya umati ya waendesha bodaboda waliojitokeza.Mmoja wa madereva aliyeshiriki zoezi hilo akiwa kwenye muonekano mpya.Mkuu wa Mkoa akiongozana na baadhi ya viongozi wa chama hicho.Sehemu ya umati waliohudhuria zoezi hilo.Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akivaa koti kama ishara kwa madereva wote ambao watapaswa kuvaa wawapo safarini.Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akijianda kuvaa Helmet.Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akiwa tayari kuvaa kofia nguvu ‘Helmet.’Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akiwa katika muonekano mpya wa madereva wa bodaboda.Mkuu
wa Mkoa akiongoza maandamano ya waendesha bodaboda yaliyoanzia viwanja
vya Biafra na kuishia viwanja wa Leaders, Kinondoni. Kopro Rioba akieleza jambo kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mheshimiwa
Paul Makonda, mapema leo amezindua Chama cha Waendesha Bodaboda na Bajaj
kwa Mkoa wa Dar es Salaam. Pia ameongoza maandamano ya waendesha
bodaboda kuanzia viwanja vya Biafra hadi viwanja vya Leaders vyote vipo
wilaya ya Kinondoni ikiwa kama ishara ya uzinduzi huo.
Uzinduzi huo umeambatana na mpango wa muonekano mpya wa madereva kwa
kuwa na kofia nguvu ‘Helment’ za kisasa na vizibao ambapo awali wengi
wao walikuwa hawana kutokana na kutomudu gharama za manunuzi.Mkuu wa mkoa ametumia nafasi hiyo kuwaomba madereva kuwa mabalozi kwa wenzao wanaovunja sheria za Barabarani kwa kupakiza abiria zaidi ya mmoja ‘Mshikaki’.
Amewaomba bodaboda kuacha kutumia vilevi wakati wanafanya kazi zao za usafirishaji.
“Tumeongeza vituo vya Bodaboda na Bajaj kushirikiana na SUMATRA ili kurahisisha usafiri katika Jiji la Dar es Salaam.” Amesisitiza mkuu huyo wa mkoa.
Comments
Post a Comment