Zombe na Wenzake Washinda Kesi, Christopher Bageni Kunyongwa
Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya
Kinondoni, SP Christopher Bageni (kushoto) baada ya kuhukumiwa
kunyongwa akiagana na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam
(RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) Abdallah Zombe (katikati).
…Akiongea jambo na aliyekuwa wakili wake baada ya hukumu kutolewa.
Polisi wakimpeleka katika chumba maalum mahakamani baada ya hukumu kutolewa.
Bageni akielekea katika chumba maalum.
Abdallah Zombe (mwenye nguo nyeupe katikati) akiwa na ndugu zake baada ya kuachiwa huru.
BAADA ya kimya kirefu, Mahakama ya Rufaa leo
imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO)
Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) Abdallah Zombe, na maofisa wenzake
wawili.Hata hivyo, mahakama hiyo imemuhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kinondoni, SP Christopher Bageni.
Zombe na wenzake walikuwa wakituhumiwa kuwaua wafanyabiashara watatu wa Mahenge Morogoro na teksi dereva mmoja wa jijini Dar es Salaam Januari 14, 2006 kwa madai kuwa walikuwa majambazi.
Hukumu hiyo imekuja baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kutatia rufaa hukumu iliyotolewa Mahakama Kuu ya Tanzania ambayo iliwaachia huru Zombe na wenzake wanne. Wafanyabiashara wa madini waliouawa katika msitu wa Pande, wilayani Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar ni Sabinus Chigumbi maarufu kama Jongo, Mathias Linkombe, Ephrahim Chigumbi na dereva wa teksi, Juma Ndugu.
Hata hivyo, DPP aliwafutia mashitaka wajibu rufani watano ambao ni Jane Andrew, Emamanuel Mabula, Michael Shonza, Abineth Salon a Festus Gwabisabi.
SOURCE:GPL
Comments
Post a Comment