MKUU WA WILAYA YA ILALA AONGOZA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUCHANGIA MAAFA YA TETEMEKO BUKOBA
Mkuu
wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akipokea kiasi cha shilingi milioni
zaidi ya milioni 6 kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara wa Kariakoo Bw.
Deo Senya wakati Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK)
walipofanya Harambee ya kuchangia wahanga wa Tetemeko la Ardhi kule
Bukoba mkoani Kagera ambapo Mkuu wa wilaya hiyo aliongoza harambee hiyo,
Kuliani ni Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala Bw. Edward Mpogolo na
katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanya Biashara Kariakoo
Bw.Philimin Lomano Chonde.
Katika
harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 13,708,000/= fedha taslimu
zilikusanywa na vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni
31564800/= jumla ya michango kwa ujumla ni shilingi milioni 45,672,800/=
harambee hiyo leo ilikuwa inazinduliwa rasmi na michango inaendelea
mpaka siku ya jumamosi ijayo ambapo ndiyo harambee hiyo itafungwa rasmi
na wafanyabiashara mbalimbali wametakiwakuendelea kuchangia kwa kupitia
jumuiya yao ya wafanyabiashara mpaka siku ya jumamosi.(PICHA NA JOHN
BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Mkuu
wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akipokeamsaada wa viatu kutoka kwa
wafanyabiashara wa kikundi cha Raha Square wafanyabiashara ambao wametoa
mchango ubwa sana wa fedha na vitu mbalimbali katika harambee hiyo.
Wafanyabiashara wa Raha Square Kariakoo wakikabidhi mchango wao wa fedha kwa mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema.
Raha Square wakikabidhi Magodoro , Nguo, Vikoi , Mashuka na vitu vingine mbalimbali katika harambee hiyo.
Wakikabidhi Suti na vitengi pamoja na mashuka katika harambee hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Ilala akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo mara baada ya harambee hiyo.
Mkuu
wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akiwahutubia wafanyabiashara na
wananchi mbalimbali waliohudhuria katika harambee hiyo.
Mfanyabiashara
Mohammed Abdallah Nofa akizungumza mara baada ya kukabidhi mchango wake
wa shilingi 500.000 kwa Mkuu wa wilaya Ilala Mh. Sophia Mjema wa pili
kutoka kulia . katika picha kulia ni Edward Mpogolo Katibu Tawala wa
Wilaya ya Ilala na Kushoto ni Katibu wa JWK Bw. Abdallah Mwinyi
Wafanyabiashara kutoka Raha Square wakikusanya michango yao ya fedha taslimu na vifaa mbalimbali kabla ya kuvikabidhi leo.
Kiongozi
wa Wafanyabiashara wauza Simu za mkononi Bw.Stanley Mwakipesile
akizungumza machache mara baada ya kukabidhi mchango wao zaidi shilingi
milioni 1.500.000 kwa mkuu wa wilaya ya Ilala katika Harambee hiyo.
Comments
Post a Comment