Skip to main content

Jacqueline Mengi Afanya Uzinduzi Wa Duka La Samani (Molocaho – Amorette)

jo6a8121
Mrembo wa taji la Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na wageni walikwa pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa duka lake la samani za ndani “Amorette” lililopo katika jengo la Village Walk gorofa ya kwanza karibu na Sea Cliff Hotel, Masaki jijini Dar es Salaam.
jo6a8110
Muonekano wa nje utaokutambulisha hili ndio duka la “Amorette”
jo6a8126
 Bi. Jacqueline Mengi akikata utepe kuzindua duka lake hilo.
jo6a8131
Ha ha ha ha, sasa mko huru kuingia wageni waalikwa kujionea yaliyomo,…..Bi. Jacqueline Mengi akifurahi jambo mara baada ya kukata utepe.
jo6a8142
Bi. Jacqueline Mengi akiongozana na baadhi ya wageni waalikwa kuingia ndani ya duka la “Amorette”
jo6a8158
Balozi Juma Mwapachu na baadhi ya wageni waalikwa wakiangalia moja ya meza ya chakula (dining table) iliyotengenezwa kwa mbao aina ya Mninga baada ya kuzinduliwa duka hilo lililopo katika jengo la Village Walk, Masaki jijini Dar.
jo6a8167
Wageni waalikwa wakiendelea kukagua samani mbalimbali katika duka hilo.
amorette
 Bi. Jacqueline Mengi akiwaonyesha mambo mazuri yaliyomo katika duka la Amorette baadhi marafiki waliohudhuria uzinduzi huo.
jo6a8196
 Bi. Jacqueline Mengi akizungumza jambo na Balozi Juma Mwapachu wakati akiwatembeza wageni waalikwa katika maeneo mbalimbali ndani ya duka lake la Amorette.
jo6a8192
Wageni waalika wakiangalia moja ya kitanda cha aina yake kinachouzwa katika duka la Amorette lililopo katika jengo la Village Walk, Masaki jijini Dar es Salaam.
jo6a8214
Sehemu maalum ya kitanda hicho ya kuhifadhia mashuka, Blanket pamoja na mito.
jo6a8229
 Bi. Jacqueline Mengi akipozi katika moja ya samani ndani ya duka lake la Amorette.
jo6a8278
 Bi. Jacqueline Mengi katika pozi matata ndani ya duka lake la Amorette.
jo6a8315
 Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua duka lake la samani za ndani la Amorette.
jo6a8227
Wanahabari na wageni waalikwa wakiwa ndani ya duka la Amorette kujionea bidhaa mbalimbali.
jo6a8201
Wageni waalikwa wakiendelea kutazama kitanda hicho cha aina yake.
jo6a8544
Sophia Byanaku akijinafasi katika moja ya samani zilizomo kwenye duka la Amorette.
jo6a8176
Mmoja wa wageni waalikwa akitazama bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa kwa mbao aina ya Mninga ndani ya duka la Amorette.
jo6a8180
Baadhi ya samani zilizomo ndani ya duka la Amorette.
jo6a8241
Balozi Juma Mwapachu (kushoto) akibadilishana mawazo na mwalikwa mwenzake kwenye uzinduzi wa duka la Amorette.
jo6a8260
Mwanadada Monica Joseph akipozi kwenye moja ya bidhaa zilizopo ndani ya duka la Amorette.
jo6a8371Bi. Jacqueline Mengi akipozi kwenye samani moja wapo inayopatikana katika duka lake la Amorette.
jo6a8505Warembo wakiwa wamepozi kwenye samani zinazopatikana katika duka la Amorette lililopo ndani ya jengo la Village Walk, Masaki jijini Dar es Salaam.
jo6a8464Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo ndani ya duka la Molocaho-Amorette.
jo6a8487
 Bi. Jacqueline Mengi akiwa kwenye picha ya pamoja na rafiki zake.
jo6a8547Bi. Jacqueline Mengi akibadilishana mawazo na baadhi ya marafiki zake.
jo6a8522
Mkurugenzi wa Dorice Mollel Foundation, Dorice Mollel (kulia) katika picha ya pamoja na Mdau Monica Joseph.
jo6a8557
 Bi. Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na Dorice Mollel.
Alhamisi ya Septemba, 15 inaingia katika historia ya mjasiriamali, Jacqueline Mengi kwa kufanya uzinduzi wa duka la samani za ndani la Molocaho Amorette likiwa na vitu ambavyo ni vya pekee kutokana na aina ya malighafi ambayo wametumia kutengeneza.
Akizungumzia duka hilo, Bi.Mengi alisema kuwa ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu ya kutaka siku moja kuwa na duka kama hilo ambalo litakuwa na samani ambazo ni ngumu kuzipata sehemu nyingine kutokana na kutengenezwa tofauti na samani nyingi ambazo zinapatikana madukani.
“Siamini kama ndoto yangu imetia, kwa kipindi cha miaka iliyopita kuna vitu nilikuwa nikitamani kuwa navyo nyumbani lakini sikuweza kuvipata nilipokuwa nikitafuta na hapo ndipo ndoto za kuwa na duka zilipoanzia,
“Nilikuwa nataka kitu cha tofauti ambacho ni ngumu kukikuta sehemu nyingine kutokana na kuwa na ubunifu wa kipekee ambao utawavutia wateja wa ndani ya nchi na nje ya nchi na ninaamini watafurahia,” alisema Bi. Mengi.
Aidha Bi. Mengi alisema kuwa bidhaa ambazo zitakuwa zikipatikana katika duka la Molocaho – Amorette zimetengenezwa na malighafi kutoka Tanzania kama mbao za Mninga na hivyo kuwataka Watanzania kuwa wazalendo kwa kutumia bidaa ambayo imetengenezwa na malighafi za Tanzania.
Mmoja wa wageni waliohudhuria halfa ya uzinduzi, Faraja Nyalandu alisema kuwa kwa kijana kama Jacqueline Mengi kuwa na duka kama hilo ni hatua kubwa ambayo vijana wengi wanatamani kuifikia, kumpongeza kwa juhudi alizozifanya lakini pia kutoa ushauri kwa wengine ambao wanataka kufanikiwa.
“Kwanza nimpongeze Jacqueline amefanya uthubutu na amefanikiwa kuwa na kitu kama hiki, juhudi yake inaonyesha kuwa  kila mtu tu anaweza  kufanikiwa kama akiongeza juhudi katika jambo analotaka kulifanya,” alisema Bi. Nyalandu.
Duka hilo la kisasa na la aina yake linapatikana Masaki karibu na hoteli ya Sea Cliff kwenye jengo la “Village Walk” gorofa ya kwanza

Comments

Popular posts from this blog