RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA, AKABIDHIWA MSAADA WA DOLA LAKI MBILI UTOKA KWA RAIS MUSEVENI WA UGANDA
Rais wa
Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi mchango wa
fedha cha dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) - takriban Tshs.
437,000,000/- taslimu uliotolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta
Museveni kwa ajili ya kusaidia waathirika watetemeko la ardhi mkoani
Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea msaada
wa fedha cha dola laki mbili za Kimarekani (USD 200,000) -takriban
Tshs. 437,000,000/- taslimu kutoka kwa Balozi wa Uganda hapa nchini
Mhe. Doroth Samali Hyuha ( wa pili kutoka kushoto) akiwa pamoja na Kaimu
Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Elibariki Maleko. Msaada huo
umetolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya
kuwasaidia waathirika wa Tetemeko la ardhi mkoani Kagera leo Ikulu
jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kusoma taarifa kuhusu Tetemeko
la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Naibu Balozi wa Kenya hapa nchini Mhe. Boniface Muhia mara baada ya
kupokea salamu za pole kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na kwa
misaada mbalimbali ya mabati 4,000 na vifaa vya majumbani ikiwemo
magodoro na mashuka ambayo inatarajiwa kuwasili mkoani Kagera kutoka
Kenya muda wowote kuanzia sasa. Katikati ni Balozi wa Uganda hapa nchini
Mhe. Doroth Samali Hyuha
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
mara baada ya kupokea msaada wa fedha dola laki mbili za Kimarekani
(takriban Tshs. 437,000,000/- ) taslimu kutoka Uganda pamoja na taarifa
ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera kutoka kwa Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
Comments
Post a Comment