Posts

Yanga yamuacha Kessy

Image
Mchezaji wa Yanga, Hassan Kessy. Wilbert Molandi, Dar es Salaam MSAFARA wa wachezaji 21 wa Yanga, asubuhi ya kesho Jumamosi utaondoka kuelekea nchini Ghana kwa ajili ya kukipiga na Medeama ya nchini humo huku wakiwaacha mabeki wao, Hassan Kessy na Mtogo, Vincent Bossou. Yanga itarudiana na Medeama katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada kutoka sare ya kufungana bao 1-1 mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Julai 16, mwaka huu. Chini ya Kocha Mholanzi, Hans van Der Pluijm, Yanga inatakiwa kushinda kwenye mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kucheza Nusu Fainali ya michuano hiyo, kinyume na hapo hali ya mambo inaweza kuwa mbaya na yawezekana wakawa wamefuta ndoto za kusonga mbele. Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, amesema msafara wao unatarajiwa kuwa na watu 30, kati ya hao, wachezaji ni 21 na viongozi tisa. Amesema msafara huo unatarajiwa kuondoka saa moja asubuhi kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JN

CHADEMA Wafungua kesi mahakama ya Afrika Mashariki dhidi ya Serikali

Image
 Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kimefungua rasmi kesi dhidi ya Serikali katika mahakama ya Afrika Mashariki kupinga zuio la kufanya mikutano ya hadhara ya kisiasa. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika aliwaambia waandishi wa habari kuwa wameamua kufungua kesi hiyo kwakuwa tamko hilo la Serikali ni kinyume cha katiba na mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na sheria ya vyama vya siasa. Mnyika ambaye aliambatana na mwanasheria wa chama hicho, John Mallya alisema kuwa wamekusanya ushahidi wa kutosha wa matamko ya katazo la kufanyika mikutano ya kisiasa na namna chama hicho kilivyozuiwa kufanya mikutano hiyo sehemu mbalimbali nchini. “Tumeleta vielelezo vya zuio lenyewe la polisi kama ushahidi wa kwamba ni kweli polisi wa Tanzania wametoa agizo kama hilo. Pili, tumeleta vielelezo vya mikutano iliyozuiwa… mikutano ya Kahama, Mahafali ya wanachuo wa Chadema kule Dodoma, Mahafali yaliyofanyika kule Moshi na mikutano mingine,”

Msiba: Tasnia ya Filamu Tanzania imepata msiba, R.I.P Mchekeshaji Kundambanda

Image
July 22 2016 ripoti zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kwa baadhi ya mastaa wa vichekesho nchini zikionyesha taarifa ya kufariki kwa mmoja kati ya wachekeshaji maarufu nchini Tanzania,   Ismail Issa Makombe  ‘ Baba Kundambanda’  kutoka kwenye maigizo ya Vituko Show. Taarifa za awali zinadai kuwa amefariki akiwa nyumbani kwao Masasi, Mtwara, endelea kuwa karibu na millardayo.com kwa taarifa zaidi.

Hii ndiyo hoteli mpya aliyofungua Chistiano Ronaldo

Image
FUNCHAL, Ureno M SHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo hatimaye ameifungua hoteli yake ya nyota tano ambayo inaonekana kuwa na ubora wa kiwango cha juu hasa katika suala la ubunifu wa majengo. Ronaldo ambaye kwa sasa yupo katika mapumziko kwenye Fukwe za Ibiza, Hispania amekamilisha mradi huo wa hoteli ambayo ipo katika Mji wa Madeira ambako ndipo nyumbani kwao. Hoteli hiyo iliyopewa jina la The Pestana CR7 Hotel, ina vyumba 48 vya kulala, gym na bwawa la kuogelea ni moja ya hoteli nne ambazo mchezaji huyo amepanga kujenga. Kwenye korido za hoteli hiyo kuna nyasi za bandia pamoja na jezi ya Ronaldo ya timu ya taifa yenye namba saba ambayo ndiyo amekuwa akiitumia. Ndani ya vyumba kuna urembo tofauti kwa kila chumba ambapo pia kuna michezo ya kwenye runinga ‘Play Station’ huku baadhi ya vyumba vikiwa na bei tofauti. Gharama ya kulala katika hoteli hiyo kwa usiku mmoja ni pauni 180 (Sh laki 5), kuna huduma ya bure ya internet, pia kuna baadh

Kisa nguo na kofia… amuua mdogo wake!

Image
  Kakamega TUKIO la aina yake limefanywa kijana Andrew Muganda (26) aliyeripotiwa kumpigwa mdogo yake Wycliffe Shitanda (23) hadi kumuua, kisa kikidaiwa kuwa alivaa nguo na kofia ya kaka yake huyo bila idhini yake, tukio lililotokeas hivi karibuni katika Kijiji cha Shamberere, Malava, Kakamega nchini Kenya. Kutokana na tarifa iliyotolewa na mama yao mzazi, Violet Lagu, Muganda limuuliza mdogo wake kwa nini alivaa nguo zake bila idhini yake, alijibu kwa jeuri. “Nina taaifa zako kuwa umekuwa ukitafuta ugomvi na mimi,” Shitanda alimjibu kaka yake. Papo hapo wawili hao walianza kupigana jambo lililopelekea Muganda kumdhibiti mdogo wake Shitanda kwa kipigo kikali hadi kupoteza maisha yake.

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA KUWAIT NA CONGO JIJINI DAR ES SALAAM.

Image
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al Najem (kulia) wakati alipokuwa akizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kuwait na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.  Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, kushoto ni Katibu Mkuu, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al Najem (kulia) masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kuwait na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.  Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, kushoto ni Katibu Mkuu, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizun

BAADA YA SERIKALI KUTANGAZA KUHITAJI VYETI UPYA KWA WAFANYAKAZI…MAGAZETI YAJAA MATANGAZO YA KUPOTELEWA KWA VYETI

Image

AMBER LULU TENA,KAMA ANA NGOMA WATAKUFA WENGI,SIRI ZAKE ZAANIKWA

Image
  Stori: Hamida Hassan, Ijumaa Dar es Salaam: Video Queen anayekuja kwa kasi Bongo, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ anadaiwa kuwa na msururu wa wanaume aliotoka nao huku ndani yake wakiwemo mastaa kibao, Ijumaa limenyetishiwa. Shosti wa Amber Lulu aliyeomba jina liwekwe kapuni alisema kuwa, kutokana na figa yake, mdada huyo amekuwa akisarandiwa na midume kibao na kila anayekuwa naye akimuacha, anahamia kwa mwingine. “Yule Amber Lulu muoneni hivihivi, figa yake asipoitumia vizuri itampoteza maana wanaume wanamshobokea kweli, sijui ni lile zigo (kalio) lake au ana kizizi maana listi yake ya wanaume ni noma, wapo mastaa kibao (anawataja kwa majina) kiasi kwamba kama ana ngoma basi wengi watakufa,” alisema mnyetishaji huyo. Ili kujua ukweli wa taarifa hizo, paparazi wetu alimvutia waya Amber Lulu na kumuuliza kama anakumbuka idadi ya wanaume aliotoka nao hadi sasa ambapo alidai kuwa hakumbuki ila akakiri kuwa mbali na watu wengine alishawahi kuwa kwenye uhusiano pia mastaa wan

Licha ya Nay wa Mitego… TRA wamhenyesha Diamond siku 7

Image
Nasibu Abdul ‘Diamond’ MUSA MATEJA, Amani DAR ES SALAAM: Imevuja! Siku chache baada ya Mbongo Fleva, Emanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kukamatwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuhusu chanzo cha utajiri wake wenye utata, mwenzake katika fani, Nasibu Abdul ‘Diamond’ naye amekumbana na kimbembe cha kuchunguzwa na TRA, Amani lina kitu mkononi. TRA ni Mamlaka ya Mapato Tanzania ambayo inajishughulisha na ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara na wananchi kwa jumla ili kuiletea nchi maendeleo kutokana na pesa hizo za kodi. CHANZO KINASEMA Kwa mujibu wa chanzo, Diamond alikumbwa na kimbembe hicho Juni, mwaka huu kabla ya Nay na kwamba, jamaa wa TRA walimvamia nyumbani kwake, Madale na kutaka aorodheshe mali zake zote ili ambazo hazijalipiwa kodi zijulikane. “Jamani, mmeandika habari za Nay kukamatwa na polisi na kuhojiwa kwa siku mbili kwa sababu ya utajiri tata. Sasa mimi nawaambia ubuyu mwingine kwamba, Diamond naye alishikwa na

WASIFU WA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI

Image
MGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI WA CCM 1.0. MAISHA YAKE Ndugu John Pombe Joseph Magufuli alizaliwa Oktoba 29, mwaka 1959 katika kijiji cha Chato, Wilayani Biharamulo katika Mkoa wa Kagera. Hivi sasa Chato ni Wilaya katika Mkoa wa Geita. Ndugu Magufuli ni Daktari wa Falsafa (PhD) ya Kemia. Ana mke na watoto saba. Alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba, 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (C.C.M). Aliapishwa na kuanza rasmi majukumu yake ya kuiongoza Tanzania tarehe 5 Novemba, 2015. Tangu ameingia madarakani, Rais Dkt. Magufuli, ameonesha kuwa ana sifa zote muhimu za uongozi. Ana dira, maono na malengo kuhusu anakotaka Taifa liende. Ana mikakati ya kutekeleza dira na maono yake. Haogopi kufanya maamuzi makini. Ana kiu ya kuona Taifa linapata maendeleo. Amejipambanua kuwa yeye ni mtetezi wa wanyonge na dhamira yake kubwa ni kuona wananchi wanapata huduma bora za jamii na kero zao zinaondoka. 2.0. ELIMU NA MAFUNZO Rais Dk

MIMBA YA JOKATE KIDOTI YAZUA BALAA,MAZITO YAFICHUKAKUHUSU KIBA

Image
Jokate na mpenzi wake, Alikiba Saleh Na Waandishi wetu Kizaazaa! Kufuatia mwanamitindo nyota Bongo na Miss Tanzania Namba 2, 2006, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kudaiwa kuwa na ujauzito wa Mbongo Fleva, Alikiba Saleh, mazito yameibuka kwa mademu waliowahi kusemekana ni ‘zilipendwa’ wa msanii huyo kusemwa kwamba, hawakuwa na uwezo wa kumzalia, Risasi Mchanganyiko linakuwa la kwanza kukudondoshea.   Chanzo makini kililiambia Risasi Mchanganyiko kuwa, warembo wanaodaiwa kuwa ni wapenzi wa zamani wa Kiba ni Gift Stanford ‘Gigy Money’, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ na Sabrina Omar ‘Sabby Angel’ kwamba hawakuwa na uwezo wa kuzaa, ndiyo maana hawakuweza kushika ujauzito wa staa huyo na kuishia kuachika tu. MSIKIE HUYU HAPA “Wapenzi wa zamani kina Gigy Money, Sabby Angel na Amber Lulu hawakuwa na uwezo wa kuzaa ndiyo maana hawakuwahi kuonekana wakiwa na ujauzito au kusikika kwamba walikuwa na mimba ikaharibika na sasa hivi hawataki hata kusikia habari za ujauzito wa Jokate hivyo tunams

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 21.07.2016

Image