Kisa nguo na kofia… amuua mdogo wake!


kakamega 
Kakamega
TUKIO la aina yake limefanywa kijana Andrew Muganda (26) aliyeripotiwa kumpigwa mdogo yake Wycliffe Shitanda (23) hadi kumuua, kisa kikidaiwa kuwa alivaa nguo na kofia ya kaka yake huyo bila idhini yake, tukio lililotokeas hivi karibuni katika Kijiji cha Shamberere, Malava, Kakamega nchini Kenya.
Kutokana na tarifa iliyotolewa na mama yao mzazi, Violet Lagu, Muganda limuuliza mdogo wake kwa nini alivaa nguo zake bila idhini yake, alijibu kwa jeuri.
“Nina taaifa zako kuwa umekuwa ukitafuta ugomvi na mimi,” Shitanda alimjibu kaka yake. Papo hapo wawili hao walianza kupigana jambo lililopelekea Muganda kumdhibiti mdogo wake Shitanda kwa kipigo kikali hadi kupoteza maisha yake.

Comments

Popular posts from this blog