Hii ndiyo hoteli mpya aliyofungua Chistiano Ronaldo

Cristiano-Ronaldo-Hotel1 FUNCHAL, Ureno
MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo hatimaye ameifungua hoteli yake ya nyota tano ambayo inaonekana kuwa na ubora wa kiwango cha juu hasa katika suala la ubunifu wa majengo. Cristiano-Ronaldo-Hotel2
Cristiano-Ronaldo-Hotel3Ronaldo ambaye kwa sasa yupo katika mapumziko kwenye Fukwe za Ibiza, Hispania amekamilisha mradi huo wa hoteli ambayo ipo katika Mji wa Madeira ambako ndipo nyumbani kwao.
Cristiano-Ronaldo-Hotel4Hoteli hiyo iliyopewa jina la The Pestana CR7 Hotel, ina vyumba 48 vya kulala, gym na bwawa la kuogelea ni moja ya hoteli nne ambazo mchezaji huyo amepanga kujenga.Cristiano-Ronaldo-Hotel
Cristiano-Ronaldo-Hotel5Kwenye korido za hoteli hiyo kuna nyasi za bandia pamoja na jezi ya Ronaldo ya timu ya taifa yenye namba saba ambayo ndiyo amekuwa akiitumia.
Cristiano-Ronaldo-Hotel6Ndani ya vyumba kuna urembo tofauti kwa kila chumba ambapo pia kuna michezo ya kwenye runinga ‘Play Station’ huku baadhi ya vyumba vikiwa na bei tofauti.
Cristiano-Ronaldo-Hotel7Gharama ya kulala katika hoteli hiyo kwa usiku mmoja ni pauni 180 (Sh laki 5), kuna huduma ya bure ya internet, pia kuna baadhi ya vyumba ambavyo kutokana na ubora wake kulala kwa usiku mmoja ni pauni 575 (Sh milioni 1.6).
Cristiano-Ronaldo-takes-his-leg-brace-off-to-dive-into-the-water-off-a-yacht-in-Ibiza8 
Hoteli nyingine ya Ronaldo ambayo inatarajiwa kufunguliwa baadaye mwaka huu itapatikana Lisbon, Ureno nyingine zitafunguliwa Madrid, Hispania na New York, Marekani.

Comments

Popular posts from this blog