WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA SOKO LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO, Tarehe 16.06.2016
WAFANYABIASHARA
wa Tanzania wametakiwa kutumia fursa za biashara zinazopatikana katika
soko la nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuuza bidhaa
zao ndani ya Jumuiya hiyo.Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga alipokuwa akizungumza
na waandishi wa habari.
“Wafanyabiashara
wanatakiwa kuchangamkia fursa ya biashara katika soko la pamoja kwa
kuwa ni haki yao na ni utekelezaji wa malengo ya Mkataba wa uanzishwaji
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kifungu cha tano ambapo ilianzishwa
itifaki ya umoja wa forodha ” ,alisema Bi. Mindi
Wafanyabiashara
hao pamoja na wasafirishaji wanaotaka kufanya biashara katika soko la
Jumuiya hiyo watatakiwa kuonesha cheti cha uasilia wa bidhaa wakati
wakiingia nchi wananchama wa Jumuiya hasa kwa wafanyabiashara wadogo
wenye bidhaa zisizozidi dola za kimarekani 2000, ambapo hawalazimiki
kuwa na wakala wa forodha.
Wanatakiwa
kufuata utaratibu kwa kufika katika kituo chochote cha forodha
kilichopo mpakani wakiwa na bidhaa zao ili wapewe cheti cha uasilia wa
bidhaa.Naye, Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji,
katika Wizara hiyo, Bw. Geofrey Mwambe, amesema ni vyema wafanyabiashara
wakatoa taarifa endapo watakumbana na vikwazo visivyo vya kiforodha
kupitia mfumo wa ujumbe mfupi kwa kuandika neno ‘NTB’ kwenda namba
15539.
Bw.
Mwambe amesema pia ,madereva wanaosafirisha mizigo kwenda nchi wanachama
watakapokutana na vikwazo visivyo vya kiforodha barabarani watoe
taarifa kwa Jeshi la Polisi kupitia namba 0713631780.
Kwa
mujibu wa Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kifungu
namba 5 ambapo Jukuiya ilianzisha Itifaki ya Umoja wa Forodha (East
African Community Customs Union) wafanyabiashara wa nchi wanachama wa
Jumuiya hiyo wana fursa za kufanya biashara kwa kuuza bidhaa zao ndani
ya nchiwanachama wa Jumuiya hiyo ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda,
Rwanda na Burundi bila kutozwa ushuru wa forodha ilimradi bidhaa zao
zimezingatia vigezo na kufuata utaratibu ulioainishwa katika itifaki
hiyo.
Japokuwa
Sudani ya Kusini imeridhia kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki bado
fursa za kufanya biashara nchini humo hazijakamilika.
Comments
Post a Comment