Posts

Glory Gideon Atwaa Taji la Miss IFM 2016

Image
Miss IFM 2016 Groly Gideon (katikati), akiwa kwenye pozi na mshindi namba mbili Nasra Muna (kushoto), huku kulia akiwa amepozi Neema Michael ambaye alinyakulia taji namba tatu. Miss IFM 2016 Glory Gideon (katikati), akiwa kwenye pozi na washindi wenzake wa pili hadi wa tano muda mfupi baada ya kutawazwa kushikilia taji hilo ndani ya Ukumbi wa King Solomon Namanga jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Mshindi namba mbili wa mashindano hayo Nasra Muna (katikati), akicheza staili ya shock ikiwa ni ishara ya kushngilia ushindi huo. Wasanii wanaounda kundi la Navy Kenzo wakitumbuiza kwenye mashindano hayo. Mamiss wote waliyoshiriki mashindano hayo wakiwa kwenye pozi la pamoja kabla ya majaji kutaja washindi watano wa kinyang’anyiro hicho. Majaji wa shindano hilo wakiongozwa na Martin Kadinda wa kwanza kushoto wakijadiliana namna ya kumpata mshindi wa taji hilo. Mgeni rasmi wa mashindano hayo ambaye ni Mwenyekiti wa Vyuo Vikuu Tanzania, Zainabu Abdalah Issa

Harambee ya Mwanafunzi Aliyepoteza Uono Akiwa Chuo Kufanyika leo

Image
Bernadetha Msigwa. Dar es Salaam: Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Mzumbe leo itafanya harambee chuoni hapo ya kumchangia mwanafunzi Bernadetha Msigwa kwa ajili ya matibabu ya macho ili aweze kuona tena. Harambee hiyo itajumuisha wanafunzi, walimu pamoja na watu mbalimbali ambao wameamua kumsaidia binti huyo. Mhadhiri wa Kitivo cha Utawala cha chuo hicho, Aloyce Gervas alisema harambee hiyo itafanyika kuanzia saa mbili asubuhi. Alisema baada ya kubaini kuwa tatizo lake lina tiba ndipo walipoanza kampeni kupitia mitandao ya kijamii: “Tunashukuru kampeni ya Kipepeo inayoendeshwa na Clouds Media na wasamaria wengine wote kwa kupokea wito wetu wa kumchangia Bernadetha. Tunatoa shukrani zetu kwa Rais John Magufuli kwa kutoa mchango wake baada ya kuona kipindi cha Kipepeo katika kipindi cha ya 360 cha kituo hicho. Akimzungumzia mwanafunzi huyo, Gervas alisema: “Kutokana na hali yake, huwa tunampatia mtihani wa kujieleza, hapo ndipo utajua ni mwanafunzi mwenye akili na

NECTA SASA KUFUNGA MITIHANI KWA KUTUMIA MASHINE.

Image
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kwa mwaka 20016/2017 mjini Dodoma.(Picha kutoka maktaba) Na Fatma Salum-MAELEZO, Dodoma. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limejipanga kuanza kufunga bahasha zenye karatasi za mitihani kwa kutumia mashine maalum ili kuondokana na hatari ya kuvuja kwa mitihani hiyo na gharama za ufungaji wa mitihani kwa kutumia mikono. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2016/2017, jana Bungeni Mjini Dodoma. Prof. Ndalichako alisema kuwa katika kuimarisha utendaji kazi wake NECTA itanunua mashine mbili za kufunga mitihani (Auto Poly Wrapping and Packing Machine) ili kuimarisha usalama wa mitihani kwa kupunguza watu wanaoshiriki kwenye maandalizi ya mitih

Kumbe House girl Alitoweka Mchana, Dada’ke Msuya Akauawa Usiku

Image
Marehemu Aneth Msuya. Siku moja baada ya kifo cha dada wa bilionea Erasto Msuya, Aneth imebainika kuwa msaidizi wa ndani aliondoka saa sita mchana kwa kuacha funguo nyumba ya jirani. Akizungumza nyumbani kwa dada wa marehemu, Mbezi Juu, mama mdogo wa marehemu Lilian Benjamin alisema msaidizi huyo alimpigia simu bosi wake mchana na kumwambia anaondoka na hataendelea na kazi. Alisema marehemu alilazimika kuomba ruhusa mapema kazini ili arudi nyumbani kwake Kibada lakini ilimlazimu kukaa nje ya nyumba kwa saa mbili baada ya kufika saa tisa alasiri na kukuta mlango umefungwa. Mama huyo alisema baada ya kusubiri kwa muda aliwauliza majirani wakamweleza kuwa walipelekewa funguo na mwanafunzi wasiyemfahamu akadai kuwa alipewa na dada mmoja aliyemuelekeza aipeleke nyumba hiyo. Haifahamiki mpaka sasa mahali alipo mfanyakazi huyo anayedaiwa kuwa mwenyeji wa Arusha. Dada mkubwa wa marehemu, Happy Msuya alisema marehemu aliwaeleza mambo hayo baada ya kupigiwa simu

WAZIRI PROFESA MAKAME ATEMBELEA DARAJA LA NYERERE NA KITUO CHA KUPIMIA MAFUTA YAINGIAYO NCHINI KUONA MAENDELEO

Image
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wawakilishi wa kampuni ya Mabey Bridge kutoka Marekani(hawapo pichani) na wadau wengine wa Ujenzi leo kuhusu mpango wa kujenga fly overs takribani tatu katika jiji la Dar es salaamu kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji. Katibu mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga akifafanua jambo kuhusu mpango wa ujenzi wa kujenga fly overs katika jiji la Dar es salaamu kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo kushoto ni muakilishi kutoka Kampuni ya Kimarekani ya Mabey Bridge Bw. Darren Keep na kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na MawasilianoProfesa Makame Mbarawa. Msimamizi Mkuu wa Daraja la Nyerere Bw. Gerald Sondo akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu maendeleo ya Daraja pamoja na changamoto wanazozikabili, katika Ziara ya kushtukiza iliyofanya na Waziri

HUYU NDO MTOTO WA MAREHEMU KEBWE ALIYEGOMA KUMPA MKONO RC MAKONDA

Image

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA JK IKULU JIJINI DAR LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete wakifurahia jambo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU

Shilingi Bilioni 3 na Mali za Bilioni 10 zataifishwa na TRA Kutoka kwa Wakwepa Kodi Bandari Kavu ya Azam

Image
Mamlaka ya kukusanya kodi TRA kupitia madalali wa Yono Auction Mart wamekusanya mali za bilioni 3 pamoja na kutaifisha mali za bilioni 10 kutoka kwa wafanyabiashara waliopitisha makontena 329 kupitia bandari kavu ya Azam bila kulipa kodi na bado wanaendelea na msako bara na visiwani. Madalali hao wamesema watu walipe kodi na watoe risiti za elekroniki la sivyo mali zitakamatwa.

WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA AKAGUA MRADI WA MABASI YA MWENDOKASI DART LEO

Image
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunzi Amina Abdallah wa darasa la sita katika shule ya msingi ya Ukombozi jijini Dar es salaam ambaye amepanda basi la Mwendo Kasi Ajentina na kushuka Manzese, Waziri Mkuu Majaliwa ametumia usafiri wa DART leo kutoka Feri kwenda Kimara Mwisho wakati alipokagua miundombinu ya usafiri huo ili kujionea mafanikio na changamoto mbalimbali zinazojitokeza mara baada ya mradi huo kuanza mwezi mmoja sasa ili ziweze kurekebishwa na kuuboresha zaidi.  Usafiri DART umekuwa mkombozi kwa wasafiri wengi wa jiji la Dar es salaam wakati wanapotoka majumbani mwao na kuelekea kazini na kurejea majumbani mwao,Katikati ni Bw. David Mwaibula aliyekuwa Mwenyekiti Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) zamani aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia

STORI YA KIFO CHA ANETH MDOGO WA BILIONEA ALIYECHINJWA

Image
May 26 kulitokea mauaji ya kutisha ya kukatwa mapanga kwa mwanadada Aneth ambaye ni ndugu wa Tajiri mmoja ambaye naye aliuliwa kwa kupigwa risasi. Aneth amepigwa mapaga na watu wasiojulika na kukimbia. Jirani wa Anetha pia mfanyakazi mwenzake anafafanua vizuri "Yaani Aneth hata siamini, jana tulikua nae kazini, kaondoka kufika nyumbani akakuta housgal katoroka, akapiga simu kwa mwenzetu akamueleza kwamba leo hatokuja ili angalie logistics. Mtoto wake ana miaka minne ndio alpo hojiwa alisema hivi jana walikuja watu watano weusi, wakavunja mlango ni majira ya mama saa tatu usiku, akakimbia chumbani, walipoingia wakamkuta mtoto wakauliza mama huko wapi akasema chumbani, wakamfuata huko mtoto hajui kilichoendelea. hadi asubuhi school bus ilipokuja alijaribu kutoka akashindwa na mwishowe iliondoka. Anafafanua: Baada ya kuona mama yake haamki ndipo alipotoka kwa jirani na kuwaita. Majirani walikwenda na kukuta Aneth akiwa amechinjwa na akiwa uchi (seem

BUNGE LAENDELEA NA KIKAO CHAKE MJINI DODOMA LEO

Image
Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza cha maswali na majibu na uchangiaji wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi leo mjini Dodoma. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Peter Mavunde ambaye akiwasalimia kwa furaha wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Dodoma leo kwenye viwanja vya Bunge. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Peter Mavunde akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi -VETA mkoa wa Dodoma nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju (katikati) akizungumza na viongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) waliolitembelea Bunge mjini Dodoma. akiwasisitiza jambo viongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) alipokutana nao nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma