WAZIRI PROFESA MAKAME ATEMBELEA DARAJA LA NYERERE NA KITUO CHA KUPIMIA MAFUTA YAINGIAYO NCHINI KUONA MAENDELEO
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na
wawakilishi wa kampuni ya Mabey Bridge kutoka Marekani(hawapo pichani)
na wadau wengine wa Ujenzi leo kuhusu mpango wa kujenga fly overs
takribani tatu katika jiji la Dar es salaamu kwa lengo la kupunguza
msongamano wa magari katika jiji.
Katibu
mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng.
Joseph Nyamhanga akifafanua jambo kuhusu mpango wa ujenzi wa kujenga fly
overs katika jiji la Dar es salaamu kwa lengo la kupunguza msongamano
wa magari katika jiji hilo kushoto ni muakilishi kutoka Kampuni ya
Kimarekani ya Mabey Bridge Bw. Darren Keep na kulia ni Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na MawasilianoProfesa Makame Mbarawa.
Msimamizi
Mkuu wa Daraja la Nyerere Bw. Gerald Sondo akieleza jambo kwa Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu maendeleo
ya Daraja pamoja na changamoto wanazozikabili, katika Ziara ya
kushtukiza iliyofanya na Waziri huyo leo jijini Dar es salaamu.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata
maelezo kutoka kwa Fundi mitambo Bw. Simon Dotto kuhusu maendeleo ya
ukarabati wa mtambo wa kupima mafuta kutoka kwenye meli kabla ya kuingia
kwenye matanki ambao uliharibika hivi karibu kutokana na mvua
iliyoambatana na upepo mkali.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata
maelezo kutoka kwa mmoja wa wahudumu wa kivuko cha Mv Magogoni kuhusu
utaratibu wa ukatishaji tiketi katika kivuko hicho leo jijini Dar es
Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata
maelezo na changamoto mbalimbali kutoka kwa abiria wanaotumia kivuko cha
Mv Magogoni leo jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Beatrice Lyimo).
Comments
Post a Comment