WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA AKAGUA MRADI WA MABASI YA MWENDOKASI DART LEO
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza
na mwanafunzi Amina Abdallah wa darasa la sita katika shule ya msingi
ya Ukombozi jijini Dar es salaam ambaye amepanda basi la Mwendo Kasi
Ajentina na kushuka Manzese, Waziri Mkuu Majaliwa ametumia usafiri wa
DART leo kutoka Feri kwenda Kimara Mwisho wakati alipokagua miundombinu
ya usafiri huo ili kujionea mafanikio na changamoto mbalimbali
zinazojitokeza mara baada ya mradi huo kuanza mwezi mmoja sasa ili
ziweze kurekebishwa na kuuboresha zaidi. Usafiri
DART umekuwa mkombozi kwa wasafiri wengi wa jiji la Dar es salaam
wakati wanapotoka majumbani mwao na kuelekea kazini na kurejea majumbani
mwao,Katikati ni Bw. David Mwaibula aliyekuwa
Mwenyekiti Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) zamani
aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo.(PICHA NA JOHN
BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia
jambo wakati Mkurugenzi wa DART Bw. David Mgwasa akisamimiana na Bw.
David Mwaibula aliyekuwa Mwenyekiti Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar
es salaam (DRTLA) zamani aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo
leo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikagua
kituo cha Kimara Mwisho mara baada ya kuwasili kituoni hapo
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza
na mwanafunzi ambaye jina lake halikufahamika mara moja wakati
alipofika kwenye kituo cha mabasi ya Mwendo kasi Kimara Mwisho leo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiuliza
swali kwa mmoja wa wafanyakazi wanaokatisha tiketi katika vituo hivyo
wakati alipokagua miundombinu ya DART leo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiangalia
utendaji kazi unavyoendelea ikiwa ni pamoja na kubaini changamoto
zinazojitokeza.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia
jambo na Mkurugenzi wa DART Bw. David Mgwasa katikati ni Mzee David
Mwaibula.
Comments
Post a Comment