Harambee ya Mwanafunzi Aliyepoteza Uono Akiwa Chuo Kufanyika leo
Bernadetha Msigwa. Dar es Salaam: Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Mzumbe leo itafanya harambee chuoni hapo ya kumchangia mwanafunzi Bernadetha Msigwa kwa ajili ya matibabu ya macho ili aweze kuona tena. Harambee hiyo itajumuisha wanafunzi, walimu pamoja na watu mbalimbali ambao wameamua kumsaidia binti huyo. Mhadhiri wa Kitivo cha Utawala cha chuo hicho, Aloyce Gervas alisema harambee hiyo itafanyika kuanzia saa mbili asubuhi. Alisema baada ya kubaini kuwa tatizo lake lina tiba ndipo walipoanza kampeni kupitia mitandao ya kijamii: “Tunashukuru kampeni ya Kipepeo inayoendeshwa na Clouds Media na wasamaria wengine wote kwa kupokea wito wetu wa kumchangia Bernadetha. Tunatoa shukrani zetu kwa Rais John Magufuli kwa kutoa mchango wake baada ya kuona kipindi cha Kipepeo katika kipindi cha ya 360 cha kituo hicho. Akimzungumzia mwanafunzi huyo, Gervas alisema: “Kutokana na hali yake, huwa tunampatia mtihani wa kujieleza, hapo ndipo utajua ni mwanafunzi mwenye akili na