Posts

RC Mwanza Atoa Saa 24 Kompyuta iliyoibwa ipatikane Ukerewe

Image
Mkuu wa mkoa wa mwanza John Mongella. Mkuu wa mkoa wa MWANZA John Mongella  ametoa saa 24 kwa kamanda wa Polisi Wilaya ya Ukerewe Ally Mkaripa, kuhakikisha wanaitafuta hadi kuipata komputa iliyoibwa usiku wa kuamkia April 22, 2016 kwenye chumba kinachotumika na mifumo ya ukusanyaji mapato  na uaandaji wa malipo ya Halmashauri (EPICOR) Mhe. Mongella ametoa agizo hilo wakati  akizungumza kwenye kikao cha kujitambulisha kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri,ambapo taarifa za awali zilionesha kutokea kwa wizi wa komputa moja iliyofungwa kwenye chumba cha mifumo ya komputa ambayo ndio hutumika kuandaa malipo mbali mbali ya halmashauri. “OCD kesho nitakwenda kanisani asubuhi, ikifika saa 8.00 mchana nataka taarifa niikute mezani kwangu, vinginevyo hatutaelewana”, amesema Mongella na kuongeza sisi tunajua nini chakufanya kama kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa lakini na wewe tumia mbinu zako kuweza kubaini wapi ilipo kompyuta hiyo. Akizungumza...

Serikali Yapangua Hoja Moja ya UKAWA

Image
SIKU moja baada ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kususa kuchangia hotuba za bajeti, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Florence Mwanri, amesema serikali haikukosea kuipa Wizara ya Ujenzi fedha zaidi ya zilizokuwa zimeidhinishwa na Bunge. Hoja hiyo ni moja kati ya tatu ambazo juzi ziliibuliwa bungeni na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe. Badala ya kuwasilisha Mpango Mbadala wa Maendeleo wa Taifa na maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu mpango wa serikali pamoja na maoni ya kambi hiyo kuhusu hotuba ya Waziri Mkuu, juzi Mbowe alisema wabunge wa upinzani watakuwa wanaingia kwenye Ukumbi wa Bunge lakini hawatachangia hotuba ya bajeti mpaka pale hoja zao zitakapojibiwa. Mbowe alidai kuwa uamuzi wao huo umetokana na Serikali kufanya kazi bila kuwa na mwongozo wa utendaji kazi kwa wizara mbalimbali, kuvunjwa kwa Katiba na sheria za nchi na kupokwa uhuru na madaraka ya muhimili wa Bunge. Mwenyekiti huyo wa Chadema na Mbunge wa Hai...

NAPE AZINDUA TAMASHA LA KIMATAIFA LA FILAMU MJINI ARUSHA

Image
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akifunua pazia kuashiria uzinduzi wa Tamasha la kimataifa la filamu la Tanzanite mjini Arusha. Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (mwenye kaunda suti ya kijivu) akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Felix Ntibenda kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na wadhamini kwenye uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite. Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite mkoani Arusha . Waziri Nape aliwaambia wadau na waigizaji wa Filamu waliohudhuria uzinduzi wa Tamasha hilo kuwa hii ni moja ya hatua kubwa kwenye historia ya filamu nchini na kuahidi Wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha haki za wasanii hazipotei wala haziliwi na wajanja. Mkurugenzi wa Tanzanite One ambao ndio wadhamini wakuu wa Tamasha, Ndugu Faisal Juma akiz...

Binti anayefanya kazi Mochwari atinga Global TV

Image
Sabrina Gharib (19) anayefanya kazi kwa vitendo kimasomo  kwenye Mochwari  ya Hospitali ya Rufaa ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani, leo ametembelea Global Publishers na kufanyiwa mahojiano na Global TV Online. Sabrina Gharib (kulia) akiwa na mama yake Asha Ramadhani wakiendelea kufanya mahojiano. Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa,  Oscar Ndauka akiongea nao jambo. Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Global wakizungumza jambo na wageni hao. Sabrina Gharib akiwa katika mapozi tofauti na wafanyakazi wa Global Publishers. BINTI mwenye miaka 19, Sabrina Gharib, anayefanya kazi kwa vitendo kimasomo  kwenye Mochwari  ya Hospitali ya Rufaa ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani, amekuwa gumzo kwa watu wanaokwenda kuchukua miili ya wapendwa wao hospitalini hapo, leo ametinga ndani ya mjengo wa Global Publishers na kufanyiwa mahojiano na Global TV Online. Akifanyiwa mahojiano kati...

UGANDA IMETANGAZA RASMI KUTUMIA BANDARI YA TANGA NCHINI TANZANIA KUSAFIRISHIA MAFUTA GHAFI YAKE.

Image
Hatimaye Serikali ya Jamhuri ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wake wa kutumia Bandari ya Tanga nchini Tanzania kusafirishia mafuta ghafi yake.  Uamuzi huo umetangazwa na Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Ushoroba wa Kaskazini uliomalizika Jijini Kampala Uganda.  Ujumbe wa Tanzania ulio kamilisha mazungumzo hayo na hatimaye kushuhudia utangazwaji wa hatua hiyo uliongozwa na Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa . Jopo la wataalamu kutoka Tanzania lililoongozwa na Mhe. Prof. Sospeter Muhongo bado wako jijini Kampala kukamilisha mpango huo wa Bomba la Mafuta Ghafi ambapo pia nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati zinatarajia kunufaika. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dar es Salaam 23 Aprili, 2015

MWANAMUZIKI NGULI WA CONGO PAPA WEMBA AFARIKI DUNIA

Image
Mwanamuziki Papa Wemba enzi za Uhai wake. Mwanamuziki nguli wa Congo Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu kama Papa Wemba amefariki dunia huko Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia leo. Habari zilizotufikia hivi punde zinasema marehemu Papa Wemba amefia hospitali alikokimbizwa mara baada ya kuanguka na kupoteza fahamu wakati akiwa katika onesho jukwaani. Papa Wemba alizaliwa June 14, 1949 huko Lubefu katika wilaya ya Sankuru nchini Congo. Alijipatia umaarufu sana kwa sauti nyororo na midundo ya Soukous ulimwenguni kote, ikiwamo Tanzania ambako amezuru mara kadhaa na kujizolea mashabiki wengi.  Papa Wemba akiwa jukwaani kwa mara ya mwisho jijini Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia  Papa Wemba aanguka na kupoteza fahamu katikati ya onesho Wafanyakazi wa huduma ya kwanza wamepanda jukwaani. Hali ilizidi kuwa mbaya wakamkibiza hospitali ambako alikata roho

RAIS MSTAAFU, MHE. DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA WANAFUNZI NA WANACHAMA WA CCM WAISHIO JIJINI BEIJING - CHINA.

Image
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akijiandaa kuzungumza na Wanafunzi na wanachama wa CCM waishio Mji wa Beijing nchini China.  Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, akizungumza na wanafunzi na Wanachama wa CCM, waishio nchini China, wakati alipokutana nao akiwa katika ziara yake nchini humo. ************************************** Na Mwandishi Wetu, Beijing China Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo tarehe 20th April 2016 amekutana na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa Tawi la Beijing ambao ni Wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu, katika Ukumbi wa Grand uliopo katika Makazi ya Viongozi ya Diaoyutai State Guesthouse jijini Beijin, nchini China. Wakisoma risala yao, Wanafunzi hao kutoka vyuo mbalimbali vilivyopo Beijin na miji ya karibu kama vile Tianjin walimuhakikishia Mheshimiwa Dkt. Kikwete kuwa wao ni waaminifu na w...

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA WENYEVITI NA MAKATIBU WA CCM WA WILAYA NA MIKOA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi wa mikoa na wilaya wa Chama Cha Mapinduzi kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar ambapo aliwashukuru kwa kazi nzuri waliofanya kipindi cha uchaguzi na kuwataka kuwa wamoja na kukiimarisha Chama. Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe.Philip Mangula akizungumza na kutoa neno la shukrani kwa niaba ya Viongozi wote wa CCM waliofanikisha ushindi wa Chama. Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akitoa neno la shukran kwa wenyeviti na makatibu wa mikoa pamoja na wilaya walioshiriki kufanikisha ushindi kwa CCM Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza nwa Wenyeviti na Makatibu wa Chama wa mikoa na wilaya wa CCM ambao walioshiriki na kufanikisha ushindi kwa Chama Cha Mapinduzi. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wa kuwashukuru viongozi wa Chama waliofanikisha ushindi kwa CCM. Baadhi ya Viongozi wa CCM wakinyo...

PICHA ZA MALKIA WA UINGEREZA AKITIMIZA MIAKA 90 HII LEO ZATOLEWA

Image
Malkia wa Uingereza ametimiza miaka 90, hii leo ambapo zimetolewa picha mbalimbali za malkia huyo akiwa na vitukuu, wajukuu pamoja na watoto wake na wenza wao. Picha hizo zenye mvuto zilizopigwa na Mmarekani Annie Leibovitz, moja wapo Malkia yupo na vitukuu vyake huku akiwa amembeba kitukuu chake cha mwisho Princess Charlotte. Malkia wa Uingereza akiwa na Prince Charles, Prince George aliyeshikwa mkono na baba yake Prince William    Picha ya pamoja ya wanafamilia ya Kifalme wa Uingereza, hapa anakosekana Prince Harry

Polepole na Hapi Waapishwa Rasmi Kuwa Wakuu wa Wilaya

Image
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Humphrey Polepole, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo. Wakuu wa wilaya za Kinondoni na Musoma wameapishwa leo baada ya kuteuliwa mapema wiki hii na Rais John Magufuli. Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa Paul Makonda amemwapisha mkuu mpya wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Salum Hapi, aliyeteuliwa Aprili 18.   Mkuu mpya wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Salum Hapi Ali Hapi amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Makonda ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mwezi uliopita. RC Makonda amempa DC huyo vipaumbele saba vya wilaya hiyo, ambavyo alisema kuwa ni pamoja na afya, haki ardhi, rushwa, kero na kushughulikia migogoro. “Natuma salamu kwa wala rushwa na mafisadi wote waliopo Wilaya ya Kinondoni, wanaopora haki za wananchi na rasilimali za nchi ili kujinufaisha wao na familia zao. Nitapambana nao usiku na mchana kuhakikisha ninashinda vita hii,” alisema Ali Salum Hapi. Naye mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo...

DIAMOND PLATINUMS MREMBO IRENE LYNN SIRI NZITO,MENGI YAFICHUKA

Image
Kuna siri nzito kati ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ au baba Tiffah na mrembo aliyejulikana kwa jina moja la Irene ‘Lynn’ ambapo watu wa karibu wanasema ‘wanatoka’. Kwa mujibu wa watu hao, Irene amekuwa akishinda kwenye Studio ya Wasafi inayomilikiwa na Diamond, iliyopo Sinza Mori jijini Dar huku wafanyakazi wote wa studio hiyo wakijua wawili hao wameshibana. “Jamani nataka kuwapa umbeya. Huu umbeya wengi hawaujui. Kuna mrembo mmoja anaitwa Irene, ndiye mtu wa Diamond kwa sasa. Diamond anampenda sana Irene. Ukienda pale studio utamkuta, muda mwingi anashinda pale. “Lakini Diamond anasema ni ndugu yake. Sasa we jiulize, Nasibu na Irene  wapi kwa wapi? Huo undugu mbona hauweki wazi kwamba ni mtoto wa nani? “Huyu Irene yupo Dar miaka yote, kama kweli ni ndugu yake mbona hajawahi kuonekana kwenye shughuli za Diamond kama wanavyoonekana Queen Darlin na Esma (dada wa Diamond)?” kilisema chanzo hicho... Kikaendelea: Lakini huwezi amini,Irene ni ki...

Ulishajiuliza unapenda nini kwa mpenzi wako?

Image
Asalaam Alaikum wapenzi wasomaji wa safu hii, bila shaka ni wazima mnaendelea vema na ujenzi wa taifa, kwa waliokutwa na mafuriko nawapa pole Mungu awape subra na wepesi Ishallah. Leo kwenye safu hii nimekuja tuongelee suala hili la wapenzi kupendana na kufikia kuwa mwili mmoja je, umewahi kujiuliza maswali kuhusiana na mwenza wako? Maswali haya yanawahusu wote. Mnatafuta nini ndani ya wenza wenu ni kitu gani mnaangalia/mnakiona ndani ya mtu unayeamua kuwa naye kama mchumba/mume/mke. Je, ni macho yake au tabasamu, ama ni muonekano wake, uchangamfu au upole, ni kitu gani unachokiona ndani ya mtu kinachokuvutia. Wengine wanavutiwa jinsi mtu anavyofikiria, au mwili wake, wewe je? Unaweza ukawa umevutiwa na kitu kimojawapo, lakini unajua uhusiano mzuri haujengwi na vitu hivi tu, kuwa na uhusiano mzuri na mwenza wako inahusisha vitu vingi sana tofauti na tabasamu lake iwe unatafuta mtu wa kuwa naye au kama tayari upo katika uhusiano hakikisha mnakubaliana vitu mu...

BREAKING NEWS: MHANDISI MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM NA WASAIDIZI WAKE WATUMBULIWA.

Image
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akizungumza na wanahabari kuhusu kumvua madaraka Mhandisi wa Manispaa hiyo,Japhery Bwigane na wasaidizi wake wawili kwa tuhuma za kusimamia ujenzi wa barabara za manispaa hiyo kwa kujengwa chini ya kiwango. MANISPAA ya Ilala jijini Dar es Salaam imemvua madaraka Mkuu wa Idara ya ujenzi, Mhandisi Japhery Bwigane na wasaidizi wake wawili kwa tuhuma za kusimamia ujenzi wa barabara za manispaa hiyo kwa kujengwa chini ya kiwango. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam wakati akitoa taarifa hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko aliwataja maofisa wengine wa idara hiyo waliosimamishwa kuwa ni Siajari Mahili na Daniel Kirigiti ambao wamehamishwa idara hiyo ili kupisha uchunguzi unaoendelea. Kuyeko alisema kikao cha Baraza la Madiwani kimefikia uamuzi huo baada ya manispaa kujiridhisha kuwa maofisa hao wamechangia kwa kiasi kikubwa ujenzi wa barabara mbovu ndani ya manispaa hiyo. Alise...