Polepole na Hapi Waapishwa Rasmi Kuwa Wakuu wa Wilaya
Wakuu wa wilaya za Kinondoni na Musoma wameapishwa leo baada ya kuteuliwa mapema wiki hii na Rais John Magufuli.
Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa
Paul Makonda amemwapisha mkuu mpya wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Salum
Hapi, aliyeteuliwa Aprili 18.
Mkuu mpya wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Salum Hapi
Ali Hapi amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Makonda ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mwezi uliopita.
RC Makonda amempa DC huyo vipaumbele
saba vya wilaya hiyo, ambavyo alisema kuwa ni pamoja na afya, haki
ardhi, rushwa, kero na kushughulikia migogoro.
“Natuma salamu kwa wala rushwa na
mafisadi wote waliopo Wilaya ya Kinondoni, wanaopora haki za wananchi na
rasilimali za nchi ili kujinufaisha wao na familia zao. Nitapambana nao
usiku na mchana kuhakikisha ninashinda vita hii,” alisema Ali Salum Hapi.
Naye mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa
Mulongo amemwapisha Humphrey Polepole kuwa mkuu wa Wilaya ya Musoma
baada ya kuteuliwa Aprili 18 kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Zelothe
Stephen aliyeteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Comments
Post a Comment