Binti anayefanya kazi Mochwari atinga Global TV

IMG_0672Sabrina Gharib (19) anayefanya kazi kwa vitendo kimasomo  kwenye Mochwari  ya Hospitali ya Rufaa ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani, leo ametembelea Global Publishers na kufanyiwa mahojiano na Global TV Online.
IMG_0694 IMG_0695Sabrina Gharib (kulia) akiwa na mama yake Asha Ramadhani wakiendelea kufanya mahojiano.
IMG_0698Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa,  Oscar Ndauka akiongea nao jambo.
IMG_0715
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Global wakizungumza jambo na wageni hao.
IMG_0687 IMG_0686 IMG_0681Sabrina Gharib akiwa katika mapozi tofauti na wafanyakazi wa Global Publishers.
BINTI mwenye miaka 19, Sabrina Gharib, anayefanya kazi kwa vitendo kimasomo  kwenye Mochwari  ya Hospitali ya Rufaa ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani, amekuwa gumzo kwa watu wanaokwenda kuchukua miili ya wapendwa wao hospitalini hapo, leo ametinga ndani ya mjengo wa Global Publishers na kufanyiwa mahojiano na Global TV Online.
Akifanyiwa mahojiano katika kipindi cha Exclusive, Sabrina aliyekuwa ameongozana na mama yake alisema kuwa hajawahi kufundishwa ujasiri na alichokuwa akifanya ni moyo wa kipekee alioumbiwa nao.

“Kwa mara ya kwanza nilipoanza kufanya kazi mochwari nilipewa maiti ya bibi, kiukweli nililia sana na sio kwamba nililia kuiona maiti ama kwa uoga bali kwa uzee aliokuwa nao yule bibi, baada ya hapo nikazoea nikawa nahudumia vizuri,’ alisema Sabrina.
Mbali na hiyo, Sabrina anayeishi Mlandizi alisema kuwa amekuwa na wakati mgumu kwa kutengwa karibu na marafiki zake wengi kutokana na kazi anayofanya.

“Nilikuwa na marafiki wengi lakini kwa sasa wengi wamenitenga kutokana na kazi ninayofanya,” alisema Sabrina.
Naye mama wa Sabrina alisema kuwa mtoto wake huyo amekuwa na kitu cha kipekee na kuwaomba wazazi wengine wawaache watoto wafanye kitu wanachokipenda.

“Mwanzoni alipokuwa akitaka kusomea kazi hii ya mochwari nilimkatalia lakini baadaye nikamruhusu, Sabrina ni mtoto pekee kwangu,” alisema mama Sabrina.
(HABARI: ANDREW CARLOS/GPL

Comments

Popular posts from this blog