Ulishajiuliza unapenda nini kwa mpenzi wako?
Asalaam
Alaikum wapenzi wasomaji wa safu hii, bila shaka ni wazima mnaendelea
vema na ujenzi wa taifa, kwa waliokutwa na mafuriko nawapa pole Mungu
awape subra na wepesi Ishallah.
Leo kwenye safu hii nimekuja tuongelee
suala hili la wapenzi kupendana na kufikia kuwa mwili mmoja je, umewahi
kujiuliza maswali kuhusiana na mwenza wako? Maswali haya yanawahusu
wote.
Mnatafuta nini ndani ya wenza wenu ni
kitu gani mnaangalia/mnakiona ndani ya mtu unayeamua kuwa naye kama
mchumba/mume/mke. Je, ni macho yake au tabasamu, ama ni muonekano wake,
uchangamfu au upole, ni kitu gani unachokiona ndani ya mtu
kinachokuvutia. Wengine wanavutiwa jinsi mtu anavyofikiria, au mwili
wake, wewe je?
Unaweza ukawa umevutiwa na kitu kimojawapo, lakini unajua uhusiano mzuri haujengwi na vitu hivi tu, kuwa na
Unaweza ukawa umevutiwa na kitu kimojawapo, lakini unajua uhusiano mzuri haujengwi na vitu hivi tu, kuwa na
uhusiano mzuri na mwenza wako inahusisha
vitu vingi sana tofauti na tabasamu lake iwe unatafuta mtu wa kuwa naye
au kama tayari upo katika uhusiano hakikisha mnakubaliana vitu muhimu
ambavyo mkividharau kisa umempenda kwa sababu ya shepu yake au ucheshi
wake vinaweza kuharibu uhusiano huko mbele ambapo ni pagumu zaidi.
Vitu unavyotakiwa kuangalia zaidi
Hivi ni baadhi ya vitu unavyotakiwa kuangalia ndani ya mwenza wako kama unataka uhusiano mzuri na kama kweli atakuwa mke au mume, epuka kuangalia vitu vya awali kama hivyo nilivyovitaja hapo.
Hivi ni baadhi ya vitu unavyotakiwa kuangalia ndani ya mwenza wako kama unataka uhusiano mzuri na kama kweli atakuwa mke au mume, epuka kuangalia vitu vya awali kama hivyo nilivyovitaja hapo.
Anakupa heshima yako, haijalishi kama yeye ni mkubwa kwako, na hapa heshima siyo salamu kama wengi mnavyodhani.
Anaheshimu maamuzi yako, kama ni katika kazi au kitu unachoamua kufanya na siyo kukucheka au kukudharau.
Hakukatishi tamaa anakuunga mkono kwenye kila jambo na kukupa moyo wa kushinda kila wakati.
Anaheshimu maamuzi yako, kama ni katika kazi au kitu unachoamua kufanya na siyo kukucheka au kukudharau.
Hakukatishi tamaa anakuunga mkono kwenye kila jambo na kukupa moyo wa kushinda kila wakati.
Hakasiriki ukijipa muda na marafiki au familia yako, unatakiwa kuwa na uhuru wa kujichanganya na watu wengine siyo yeye tu.
Anasikiliza mawazo
yako na kukushauri
Mnashea vitu unavyovipenda kama vile kuangalia muvi, aina ya muziki, kucheza. Angalau muwe na kitu kimoja ambacho wote mnapenda ili muwe na kitu cha kufanya pamoja, vitu vingine mnaweza kutofa-utiana haina shida kwa sababu hata mapacha waliozaliwa pamoja kuna wakati huwa wanato-fautiana lakini iwe kuna kitu mnaendana ambacho mtashiriki pamoja.

Mpenzi huyo asiwe mkaidi kwa kila kitu unachomwambia, hii inawahusu wapenzi wote si wanaume ama wanawake tu.
Awe anaheshimu mipaka yako, siyo atake kujua kila kitu chako kama vile kukagua simu au wapi unapokuwa saa 24, kama mpo katika uhusiano mnatakiwa mheshimiane maana mwanzo wa kufuatiliana saa zote ndiyo mwanzo wa ugomvi usiyoisha.
Asiogope kukuambia anavyojihisi, hii itawasaidia hata pale mtakapokuwa na matatizo ili muweze kusuluhisha mambo yenu, itawaondoa kwenye hali ya kila mtu kumuwekea mwenzake kinyongo.

Kumbuka uhusiano unahusisha watu wawili,
wewe na patna wako muwe na usemi ndani ya uhusiano wenu na msiogope
kuambiana mnachohisi na kusikilizana pia.
Ndani ya kila uhusiano kuna kugombana,
hiki ni kitu cha kawaida kabisa. Wale mnaowaona wana furaha katika
uhusiano wao wameweza kujua jinsi ya kuyamaliza matatizo yao.
Usimpende mtu kwa sura, fedha, uvaaji wake bali iwe kwa mapenzi ya dhati.
Usimpende mtu kwa sura, fedha, uvaaji wake bali iwe kwa mapenzi ya dhati.
Comments
Post a Comment