RAIS MSTAAFU, MHE. DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA WANAFUNZI NA WANACHAMA WA CCM WAISHIO JIJINI BEIJING - CHINA.


Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akijiandaa kuzungumza na Wanafunzi na wanachama wa CCM waishio Mji wa Beijing nchini China.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, akizungumza na wanafunzi na Wanachama wa CCM, waishio nchini China, wakati alipokutana nao akiwa katika ziara yake nchini humo.
**************************************
Na Mwandishi Wetu, Beijing China
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo tarehe 20th April 2016 amekutana na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa Tawi la Beijing ambao ni Wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu, katika Ukumbi wa Grand uliopo katika Makazi ya Viongozi ya Diaoyutai State Guesthouse jijini Beijin, nchini China.

Wakisoma risala yao, Wanafunzi hao kutoka vyuo mbalimbali vilivyopo Beijin na miji ya karibu kama vile Tianjin walimuhakikishia Mheshimiwa Dkt. Kikwete kuwa wao ni waaminifu na wazalendo kwa Taifa lao na kwamba wako tayari kurudi nyumbani na kutumia elimu zao katika kuhakikisha kuwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanafikiwa.

Katika mazungumzo na Wanachama hao, Mhe Kikwete amewakumbusha jukumu kubwa lililo mbele yao la kujenga Chama na kulijenga Taifa la Tanzania, katika hotuba yake ameeleza kuwa China imefanya Mapinduzi makubwa katika maendeleo na kuboresha ustawi wa watu wa nchi hiyo, hivyo kuwataka kujifunza na kuchukua maarifa ya China na kuyatumia wakirudi nchini ili kufanikisha Mapinduzi makubwa ya Kiuchumi na maendeleo kwa ujumla.

 Mheshimiwa Kikwete na Ujumbe wake wanatarajia kutembelea Jimbo la Fu Zhou hapo kesho na kushuhudia maendeleo makubwa yaliyosimamiwa na Katibu Mkuu wa CCP na Rais wa Serikali ya watu wa China Mhe Xi Jinping, pamoja na kufanya mazungumzo muhimu na Viongozi wa Chama Cha Kikomunisti cha China {CCP} katika jimbo hilo.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, akizungumza na wanafunzi na Wanachama wa CCM, waishio nchini China, wakati alipokutana nao akiwa katika ziara yake nchini humo.
Picha ya pamoja baada ya mazungumzo yake na wanaccm na wanafunzi wwatanzania waishio China.

Comments

Popular posts from this blog