Posts

MWAMVITA MAKAMBA AJIBU TUHUMA ZA MANGE KIMAMBI,ASEMA JANUARY MAKAMBA HAHUSIKI,MSIKILIZE HAPA

Image
January hausiki na kashfa zinazosambazwa mitandaoni. Hao ni matapeli na wameamua kumtumia tapeli mwenzao huyo anayejiita wa kitaliano. Mahusiano yangu, masuala yangu binafsi hayapaswi kuhusianishwa na kaka yangu January. Mimi nina maisha yangu na yeye ana maisha yake binafsi, mimi nina kazi zangu na yeye ana kazi zake. Puuzeni upuuzi huo unaosambazwa kwa sababu ni wa kupika Kuniuliza Leading Questions halafu kunirekodi ili unilishe maneno ni upuuzi wa kupuuzwa. Mwamvita Makamba

Lulu, Richie washinda Tuzo ya MVCA

Image
Please join me to Salute another Tanzanian hero hapa Lagos Super Star Lulu Michael   kwa kushinda  tuzo ya filamu bora Afrika Mashariki (Best Movie – East Africa) kupitia Mapenzi. Muigizaji huyo alijikuta akilia kwa furaha wakati akishukuru kushinda tuzo hiyo.at "2016 AFRICA MAGIC VIEWERS CHOICE AWARDS"  ....SALUTE SISTER and BRO. RICHIE NA MUNGU AIBARIKI TANZANIA!   Staa wa Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiongea jambo baada ya kushinda Tuzo ya Africa Magic Viewers Choice (MVCA) zilizofanyika Lagos, Nigeria. Akiwa na tuzo yake. Akifanya mahojiano. Muonekano wa ndani ya ukumbi.  Wasanii wa uigizaji Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ (kulia), Single Mtambalike ‘Rich Richie’ (kushoto) wakiwa Muongozaji filamu anayechipukia kwa kasi, Honeymoon Mohammed (katikati).

RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MAZISHI YA KAKA WA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE KIJIJINI MSOGA

Image
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016. Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiweka mchanga kwenye kaburi la Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani. Mzee Selemani Kikwete alikuwa kaka mkubwa wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Rais wa awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi wakimsikiliza kwa Makini Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifafanua jambo huko Msoga Mkoani Pwani. Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimfafanulia jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya mazishi ya Kaka yake Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani. Rais wa Jamhuri ya Muungano

DC -PAUL MAKONDA AZINDUA VITAMBULISHO VYA WALIMU KUPANDA DALADALA BURE JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Image
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akimvika kitambulisho Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani, Beatrice Mhina Dar es Salaam leo asubuhi, baada ya kuvizindua vitambulisho hivyo vitakavyotumiwa na walimu kupanda daladala bure wakati wa kwenda kazini kufuatia mpango aliouanzisha wiki iliyopita wa kuwasaidia walimu hao. DC Makonda akimfika kitambulisho Mwalimu Gideon Mwenenyi. DC Makonda akimvika kitambulisho, Mwalimu Ramadhani Korowelle. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wananchi na walimu wakati wa uzinduzi wa vitambulisho hivyo. Ofisa Elimu wa Sekondari wa wilaya ya Kinondoni, Rogers Shemwelekwa (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo. Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Turiani, Alpherio Nchimbi (kushoto), akizungumza kwenye uzinduzi huo. Walimu na viongozi wengine wakiwa kwenye hafla hiyo Wananchi na walimu wakiwa kwenye uzinduzi huo. Wananchi na walimu wakiwa kwenye uzinduzi huo. Mwali

NAPE NNAUYE:TUTUMIE UTAMADUNI WETU KUJENGA NCHI

Image
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipiga ngoma alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa Golden Jubelee Towers alipokuja kushiriki katika uzinduzi wa Video mpya ya Mshairi Mrisho Mpoto inayoitwa Sizonje .Wengine Pichani ni Mrisho Mpoto,Dr Mwaka na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa Bi leah Kihimbi. Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye Nape Nnauye akizindua rasmi video ya Sizonje,Kushoto kwake ni Mrisho Mpoto. Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiinadi video ya Sizonje kwa wadau mbalimbali waliofika kushuhudia uzinduzi huo.Nape aisema video hiyo inawakilisha serikali ya awamu ya tano na utumbuaji wa majipu. Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimkabidhi cheti cha pongezi kwa Msichana Butogwa Charles Shija aliyeongoza kitaifa katika mtihani wa kidato cha nne. Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimkabidhi cheti cha pongezi kwa Co

YATAMBUE MADHARA YA KUTOSHIRIKI TENDO LA NDOA KWA MUDA MREFU ( WANANDOA)

Image
kwa kawaida kama wewe si mgonjwa wa aina yoyote ile, kwa maana ya ugonjwa ku-offset system ya mwili, madhara ya kutofanya tendo la ndoa kwa muda mrefu ni makubwa kuliko unavyofikiria as long as upo katika active range of age! madhara yapo ya Negative na positive. Mfumo wa fahamu (central novous system) hutumia zaidi tendo la ndoa ku-radiate energy inayowezesha ubongo pamoja na mifumo mingine ya mwili kufanya kazi zake vizuri bila msongo. Suala hapa si lazima uk*e na u*me kukutana na kuingiliana (penetration) ila tu stimulation(msisimko) inayofikisha mtu kileleni (orgasms). kwahiyo, nature(asili) inataka mke na mme kufanikisha zoezi hili maana ni jambo muhimu kama ilivyo kutoka jasho mwilini maana sio tu mwili unaondoa uchafu ndani lakini pia inacontrol joto la mwili (cooling effect). Anayesema amekaa zaidi ya mwaka na hana madhara.., well sikatai wala sikubali maana hatuna ushahidi nalo lakini zipo njia nyingi mbadala kama kutumia s*x toys, dildo(vibrant

AY AWATOLEA UVIVU TCRA

Image
Ambwene Yessaya ‘AY’ amethibitisha kupokea taarifa ya kufungiwa kwa video ya wimbo ‘ Zigo remix’ aliyomshirikisha Diamond Platnumz. Akizungumza na 225 katika kipindi cha XXL cha Clouds FM, Jumatatu hii, AY amesema alipokea barua yenye amri hiyo kutoka kwa rafiki yake ambae anafanya kazi katika chombo kimoja cha habari. “Sijaelewa maadili gani kwa sababu kama maadili niliyokosea mimi ni kushoot kwenye swimming pool, na kama kwenye swimmig pool watu nimevalisha jeans au maturubai hapo nitakuwa nimekosa maadili,” alisema AY. “Mavazi ya kwenye swimming pool yako kila mahali, hata kwenye taarifa za habari (Michezo) wanaonyesha waogeleaji, kama hiyo pia ni kukiuka maadili ni sawa. Inashangaza mamlaka zetu wanafocus kwenye kufungia nyimbo zetu na kuacha video za nje. Sijawahi sikia muziki wa Kenya, Uganda au Marekani umefungiwa, kama wanaona nyimbo za Nicki Minaj zina maadili halafu Zigo ya AY haina maadili baasi unaacha tu iwe hivyo ,” aliongeza AY. Pia AY alise

Diamond kakutana na Kanye West Marekani

Image
Yoyote ambae anaufuatilia muziki wa Kanye West akikutana nae hawezi kuacha kupiga nae picha. Diamond alisafiri kuelekea Marekani Las Vegas kwa ajili ya kufanya  show, ambapo kwenye maelezo ya hii picha, ilionekana wakati huo alikuwa Los Angeles . Kwa ninavyo fahamu Diamond anakuwa mtanzania mwingine, aliyepiga picha na Kanye West , ambapo Vanessa Mdee amewahi kukutana na Kanye West na kuongea nae. Hapa ni Vanessa Mdee kulia alipokutana na Kanye West

Fahamu vyakula vya kuondoa gesi tumboni

Image
WATU wengi wamekuwa wakihangaika sana na matumbo yao kujaa gesi na pengine kuvimba. Leo nakuletea baadhi ya vyakula vya kula ili kuondoa hili tatizo. Kwa njia moja au nyingine, unajikuta tumbo limechafuka kwa kujaa gesi, kuuma na hata kuunguruma, unahisi unahitaji kunywa dawa ili litulie. Katika makala ya leo utajifunza njia bora ya kutuliza mchafuko wa tumbo kwa kutumia vyakula badala ya dawa za kisasa ambazo hutuliza dalili na haziondoi tatizo. CHANZO Kabla ya kukimbilia kwenye tiba, ni vizuri kwanza kujua chanzo cha tatizo na katika hili unahitaji kujua ni vyakula gani ukila vinasababisha matatizo ya tumbo. Aina ya vyakula inaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu lakini kuna aina ya vyakula vinajulikana zaidi kusababisha matatizo ya tumbo. Vyakula na vinywaji vinavyochangia tumbo kujaa na ukosefu wa choo kwa muda mrefu huwa ni soda, ulevi (hasa bia), vyakula vyenye mafuta mengi na vyenye chumvi nyingi. Vyakula hivyo vinapoingia tumboni, huwa na tabia ya kuchelewe

Benki Kuu ya Tanzania yawaka moto!

Image
Jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Najuwa wajuwa, Lakini mimi nakujuza zaidi ASUBUHI ya Julai 5, 1984, wakazi wa Dar es Salaam waliamka kwa mshangao baada ya kusikia na kuliona jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) likiwa linaungua kwa moto uliokuwa umesambaza moshi mkubwa na mzito juu ya anga la mji  huo ulio ufukweni mwa Bahari ya Hindi. Tukio hilo lilitokea kiasi cha miaka 32 iliyopita, wakati wa utawala wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo, kama kawaida, Watanzania waliokuwa na kazi na ambao hawakuwa na kazi,  walifurika maeneo jirani ya jengo hilo ambalo ndilo ‘mama wa fedha’ za nchi hii na kushuhudia likiwaka moto huku magari kibao ya zimamoto na wafanyakazi wake wakihangaika kuudhibiti. Kama kawaida pia, majeshi ya usalama yalikuwa yamefurika eneo hilo ili kuhakikisha hapatokei purukushani yoyote wakati wa kupambana na janga hilo. Kwa ufahamisho tu ni kwamba jengo lililoungua ni lile  ‘orijino’, yaani jengo la mwanzo kabisa la benki hiyo lililofunguliwa J