NAPE NNAUYE:TUTUMIE UTAMADUNI WETU KUJENGA NCHI
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipiga ngoma
alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa Golden Jubelee Towers alipokuja
kushiriki katika uzinduzi wa Video mpya ya Mshairi Mrisho Mpoto
inayoitwa Sizonje .Wengine Pichani ni Mrisho Mpoto,Dr Mwaka na Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Sanaa Bi leah Kihimbi.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye Nape Nnauye
akizindua rasmi video ya Sizonje,Kushoto kwake ni Mrisho Mpoto.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiinadi video ya
Sizonje kwa wadau mbalimbali waliofika kushuhudia uzinduzi huo.Nape
aisema video hiyo inawakilisha serikali ya awamu ya tano na utumbuaji wa
majipu.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimkabidhi cheti
cha pongezi kwa Msichana Butogwa Charles Shija aliyeongoza kitaifa
katika mtihani wa kidato cha nne.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimkabidhi cheti
cha pongezi kwa Congcong Wang aliyeshika nafasi ya pili kitaifa katika
mtihani wakidato cha nne.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimkabidhi cheti
cha ushujaa kwa kijana Salmin Selemani ambae alifanya vibaya katika
mtihani wa kidato cha nne lakini hakukata tamaa na kujitokeza hadharani
ili asaidiwe,Waziri Nape amejitolea kumwendeleza kijana uyu.Picha na
Daudi Manongi.
…………………………………………………………………………………………………………
Na Daudi Manongi-WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye amewataka watanzania kutumia utamaduni wetu kujenga nchi yetu.
Waziri
nape ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa video ya mshairi Mrisho Mpoto
mbele ya wadau mbalimbali wa sanaa kutoka kila kona ya jiji la Dar es
Salaam waliofurika kuangalia uzinduzi huo ulioendana sambamba na mada
kubwa mbili za utamaduni na lugha na kauli mbiu ya Kufeli elimu sio
mwisho wa maisha.
“Serikali
ya awamu ya Tano imejipanga vyema katika kutumia utamaduni wa nchi yetu
kushape vijana wetu wawe na morali,wajitambue ili wafike
mbali,tutatumia utamaduni huu kujenga nchi yetu kikamilifu kwani ni
silaha tosha kuvutia hata nchi nyingine.Maisha sio rahisi,ni
kuvumilia,kutokata tamaa na kuweka malengo.Safari tumeianza na tutafika
mbali”Alisema Nape.
Pia
Waziri uyo aliwataka watanzania kumuunga mkono Mrisho mpoto na
kutomkatisha tamaa kwani anamsaidia rais wa awamu ya Tano Mhe.John Pombe
Magufuli katika kutumbua majipu.Mbali na hilo alimshauri Mrisho mpoto
kwenda mikoani kwani hata uko kina Sizonje wapo wengi muwaonyeshe kwamba
iko njia kwa watu waliokata tamaa.
Kwa
upande wake Mrisho mpoto aliwasii watanzania kujenga taifa letu na pia
tujenge Kiswahili na kukitumia kama ajira kwani ni lugha ya sita kwa
sasa duniani.
“Lazima
tujue kwamba Kiswahili ni lugha ya kibiashara,tuangalie fursa zilizopo
kupitia Kiswahili kujipatia ajira kwani nchi kama Namibia,Zimbabwe
wamepokea Kiswahili na wanaitaji kufundishwa zaidi na kwa namna hii izi
zote ni fursa kwani lugha imekuwa bidhaa sasa”Alisema Mpoto.
Wakichangia
katika mjadala uliopewa jina “kufeli elimu sio kufeli maisha” Bw.Ruge
Mutahaba alisema kufeli darasani kusikuzwe na kuwataka vijana
kutengeneza maono mapema kwani yatakuwa ndio mwongozo wa maisha yao yote
na yatawafanya vijana kutokata tama mapema.
“Vijana
Mjifunze kuwasiliana,muwe wabunifu,mjifunze kuwa na utaratibu wa
kujifunza kitu kipya kila siku,pia mtengeneze jamii ya watu ambao ni
watatua matatizo na sio watumikaji tu kwani kwenye matatizo ndo kwenye
fursa zote,msiiachie serikali pekee kushughulikia huduma za jamii bali
tumieni mwanya huo kuanzisha za kwenu”Alisema Ruge.
Naye
mwakilishi kutoka TBL Bw George Kavishe aliwataka vijana kujua mihimili
yao pamoja na uwezo wao na kwa kufanya ivyo watakuwa wamejua wapi
wanacho na nini kinafaa kufanya ili kuboresha maisha yao.
Mjadala
huo pamoja na uzinduzi wa video ya sizonje uliambatana na waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na michezo Mhe.Nape kuwapa vyeti vya pongezi na
ushujaa vilivyoandaliwa na Mrisho Mpoto wanafunzi waliofanya vizuri na
wale waliofanya vibaya katika mtihani wa kidato cha nne.
Comments
Post a Comment