DC -PAUL MAKONDA AZINDUA VITAMBULISHO VYA WALIMU KUPANDA DALADALA BURE JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul
Makonda (kulia), akimvika kitambulisho Mkuu wa Shule ya Sekondari ya
Turiani, Beatrice Mhina Dar es Salaam leo asubuhi, baada ya kuvizindua
vitambulisho hivyo vitakavyotumiwa na walimu kupanda daladala bure
wakati wa kwenda kazini kufuatia mpango aliouanzisha wiki iliyopita wa
kuwasaidia walimu hao.
DC Makonda akimvika kitambulisho, Mwalimu Ramadhani Korowelle.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wananchi na walimu wakati wa uzinduzi wa vitambulisho hivyo.
Ofisa Elimu wa Sekondari wa wilaya ya Kinondoni, Rogers Shemwelekwa (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Turiani, Alpherio Nchimbi (kushoto), akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Walimu na viongozi wengine wakiwa kwenye hafla hiyo
Wananchi na walimu wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wananchi na walimu wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mwalimu Happyness Mailo (kushoto), akimshukuru DC Makonda kwa kuwawezesha mpango huo.
Mwakilishi wa wananchi, Ahmed Muhonga akimshukuru DC Makonda.
Mshairi, Msafiri Himba akitoa burudani kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani, Beatrice Mhina akitoa neno la shukurani kwa DC Makonda.
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul
Makonda amezindua vitambulisho vitakavyotumiwa na walimu kupanda
daladala bure wakati wakitoka nyumbani kwenda kazini.
Katika hatua nyingine Makonda
ameziomba sekta mbalimbali nchini kushiriki katika kutoa mawazo yao ya
maendeleo ili taifa lizonge mbele badala ya kuwa watizamaji.
Makonda aliyasema hayo Dar es Salaam
jana mbele ya wazazi na walimu wa Shule ya Sekondari ya Turiani wakati
akizindua vitambulisho hivyo vitakavyotumiwa na walimu wa wilaya yake
kupanda daladala bure kufuatia mpango aliouanzisha wiki iliyopita wa
kuwasaidia walimu hao.
"Nawaomba watanzania na sekta
mbalimbali kuwa na mawazo ya maendeleo ambayo yatawekwa mezani na
kuyafanyia kazi jambo litakalo msaidia Rais wetu Dk.John Magufuli katika
kuliinua taifa kiuchumi badala ya kumuachia kila kitu akifanye yeye"
alisema Makonda.
Makonda alitoa mwito kwa makondakta
wa daladala kutoa ushirikiano kwa walimu hao kesho wakati watakapoanza
kupanda magari yao huku wakijua walimu ndio waliowafundisha na kufikia
hatua hiyo ya kazi walizonazo.
Ofisa Elimu wa Sekondari wa Wilaya
hiyo, Rogers Shemwelekwa aliwaomba wananchi hao na walimu kuendelea
kuunga mkono jitihada za Makonda za kuwaletea maendeleo na kumuombea kwa
mungu badala ya kumbeza kwani kazi hizo anazozifanya ni kwa ajili ya
wananchi.
Comments
Post a Comment