RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MAZISHI YA KAKA WA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE KIJIJINI MSOGA
Rais
Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa
mazishi ya kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi
kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5,
2016.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiweka mchanga kwenye
kaburi la Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani. Mzee
Selemani Kikwete alikuwa kaka mkubwa wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Rais wa
awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi wakimsikiliza kwa Makini Rais
Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifafanua
jambo huko Msoga Mkoani Pwani.
Rais
Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimfafanulia jambo
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya mazishi ya
Kaka yake Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani
Pwani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akimfariji Mjane wa Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa
mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo
Machi 5, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimfariji Mjane wa Marehemu Mzee
Selemani Mrisho Kikwete na wanafamilia, wakati wa mazishi kijijini
Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Mama Janeth Magufuli, mke wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
pamoja na Mama Salma Kikwete wakiwa msibani kwa kaka yake Rais Mstaafu
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, MarehemuMzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati
wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo
Machi 5, 2016. Wengine kutoka kushoto ni Mama Asha Bilali, Mama Khadija
Mwinyi, Mama Sitti Mwinyi, Mama Asha Seif Ali Iddi,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akipokea hela ya utani toka kwa Mbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete
wakati wa mazishi ya Baba yake Mkubwa Mzee Selemani Mrisho Kikwete,
kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5,
2016 wanaoshuhudia ni Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Rais
wastaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mhe. Benjamin Mkapa, Alhaj Ally
Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe John Malecela. Katika utamaduni
wa Kitanzania Wakwere na Wasukuma ni watani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akimkabidhi hela ya utani kwa mkaazi wa Chalinze ambaye ni Muskumu Bwana
Luhende baada ya kuipokea toka kwa Mbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani
Kikwete wakati wa mazishi ya Baba yake Mkubwa Mzee Selemani Mrisho
Kikwete, kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo
Machi 5, 2016 wanaoshuhudia ni Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein,
Rais wastaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mhe. Benjamin Mkapa, Alhaj Ally
Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe John Malecela. Katika
utamaduni wa Kitanzania Wakwere na Wasukuma ni watani.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinayang Bw. Khamis Mgeja akiongea
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli na Rais MStaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa Mazishi ya
Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete, kijijini Msoga, Chalinze,
wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akimpa pole Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufiwa na kaka
yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga,
Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016PICHA NA
IKULU
Mama Janeth Magufuli, mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Rais Mstaafu Dkt Jakaya
Mrisho Kikwete kwa kufiwa na kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete,
wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa
Pwani leo Machi 5, 2016
Kada wa Chadema Hamis Mgeja akimsalimia Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.
John Pombe Magufuli kabla ya mazishi ya Marehemu Mzee Selemani Mrisho
Kikwete huko Msoga mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na
Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba kabla ya mazishi ya Marehemu Mzee
Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani.PICHA NA IKULU
Comments
Post a Comment