Posts

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS KENYATTA NA RAIS KAGAME

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, kando ya Mkutano Mkuu wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Mkoani Arusha, ambapo viongozi hao wamekubaliana kuimarisha mahusiano hususani katika masuala ya kiuchumi. Baadhi ya maeneo waliyokubaliana kutilia mkazo katika mahusiano hayo, ni pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo inayounganisha nchi mbili ikiwemo ujenzi wa miundombinu, kukuza biashara na kuzalisha ajira kupitia viwanda.Rais Uhuru Kenyatta amesema amefurahishwa sana kuona Rais Magufuli yupo tayari kuhakikisha nchi ya Kenya na Tanzania zinakuwa karibu, na miradi y

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS KENYATTA NA RAIS KAGAME

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.PICHA NA IKULU.

Kiwanda Bubu Cha Kutengeneza Pafyumu Feki Chakamatwa Dar es Salaam

Image
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wamekamata kiwanda bubu kinachotengeneza pafyumu bandia kilichopo eneo  Tuangoma, mtaa wa Goroka Wilala ya Temeke. Kukamatwa kwa kiwanda hicho kinachotengeneza pafyumu aina ya SAME,  kunatokana na TFDA kupata taarifa kutoka kwa wananchi kuwa  kuna shehena kubwa  ya pafumu hizo katika duka moja la vipodozi lililopo Sinza kwa Remmy wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari  leo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hiiti Sillo alisema TFDA kanda ya mashariki baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa kiwanda hicho kutoka kwa wasamaria wema, walifanya ukaguzi katika duka hilo la vipodozi na kukamata  chupa 5,350 za pafyumu aina ya  SAME zenye thamani ya Sh 107 milioni. “Februari 23,mwaka huu tulifanya ukaguzi katika duka hilo lililopo Sinza kwa Remmy na kukuta pafyumu  5,350 ambazo zinauzwa Sh 20,000 kwa chupa moja ya pafyumu na pia tuligundua kuwa duka na pafyumu hizo zilikuwa hazijasajiliwa

RAIS MAGUFULI AMTUMIA SALAMU ZA RAMBIRAMBI RAIS MSTAAFU KWA KUKIWA NA KAKA YAKE

Image
Mzee Seleman Kikwete enzi za uhai wake

Shamsa: Siwezi Kumhukumu Nay

Image
S TAA wa Bongo Muvi, Shamsa Ford kwa mara ya kwanza ameibuka na kuiongelea Ngoma ya Shika Adabu Yako iliyoimbwa na Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kuwa kamwe hawezi kumhukumu Nay kwa maneno aliyoimba. Shamsa Ford Akigonga mbili-tatu na Showbiz, Shamsa aliyewahi kubamba na Filamu ya Chausiku alisema kuwa aliusikia wimbo huo uliowachana mastaa wengi wa Bongo Muvi na kwamba bado hajajua kinachomfaidisha Nay kupitia wimbo huo. “Namuacha kama alivyo na kamwe siwezi kumhukumu kwa kile alichokiimba labda kwa upande wake aliona ni sawa,” alisema Shamsa. Katika Wimbo wa Shika Adabu Yako, Nay amewachana mastaa wa Muziki na Bongo Muvi ambao ni Shetta, Ommy Dimpoz, Ray, Niva, Wema Sepetu na wengine wengi jambo lililosababisha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuufungia wimbo huo kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili, kashfa, uchochezi na kudhalilisha watu. Chanzo: GPL

Fahamu: Osama aliacha dola milioni 29 kufadhili Jihad

Image
Kiongozi wa kidini wa mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda Osama Bin Laden aliacha urathi wa dola milioni 29 kufadhili Jihad alipouawa mwaka 2011. Hayo ni kwa mujibu wa wasia wake iliofichuliwa leo. Aliihimiza familia yake kuheshimu waysia wake na kuwashauri ''watumie mali yake yote kuendeleza jihad'' Mali yake na wasia wake ni miongoni mwa maelfu ya stakabadhi muhimu zilizofichuliwa hii leo na maafisa wa Marekani. Aidha Bin Laden alimtaka babake amtunzie mke na wanawe endapo ataaga dunia. Kiongozi huyo wa mtandao wa kijihad wa Al Qaeda aliuawa na majeshi ya Marekani mwaka wa 2011 katika shambulizi la kufumania lililotekelezwa ndani ya Pakistan. source :rahatupu.us

ALICHO ANDIKA MASANJA MKANDAMIZAJI MALA BAADA YA KUSALIMIANA NA RAIS MAGUFULI

Image
Ukisalimiana na mkuu wa nchi lazima ucheki pembeni kidogo, maana anaweza kuona kachunusi akadhani jipu. Kauliza nguo bei gani, nikasema tumegaiwa kanisani. Maana angeweza kusema hela umetoa wapi na risiti ya mashine ya TRA ya manunuzi iko wapi

Mtoto wa Odinga amekiri kuwa alikosea alipodai kuwa bonde la Olduvai Gorge liko Kenya.

Image
Mwanawe aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga, Rosemary, amekiri kuwa alikosea alipodai kuwa bonde la Olduvai Gorge liko Kenya ilhali liko Tanzania. ''Bonde la Oldupai ama Olduvai liko Tanzania, nimekubali kuwa nilikosea nilipokuwa nikihutubia mkutano wa viongozi wa vijana kutoka kote duniani nikiwa New York Marekani(International Young Leaders Assembly). ''Nahisi kama ambaye nimewakosea ndugu zangu kutoka Tanzania''. ''Nia yangu ilikuwa ni kusema kuwa nilipokuwa mdogo nikienda shuleni nilifunzwa kuwa fuvu la mtu wa kale lilipatikana Olorgesaiile eneo la Kajiado. Nisemeje ,,nawaombeni radhi Watanzania. Olduvai Gorge iko salama wala haijanyakuliwa na kenya 'Katika ile hali ya undugu naomba kuwanyoshea mkono wa amani kwa sababu mwisho wa siku Afrika mashariki ndio kitovu cha ubinadamu'' alisema bi Odinga kupitia mtandao wake wa Instagram. Tamko lake kuhusiana na bonde hilo la Olduvai (Oldupai) lililoko Tanzania l

MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE 02.03.2016

Image

Polisi Yaua Majambazi Watatu....Baada ya Kupekuliwa Walikutwa na Ujumbe wa Kamanda Suleiman Kova

Image
Watu watatu wanaosadikiwa kujihusisha na vitendo vya kigaidi na ujambazi wameuawa katika majibizano ya risasi na polisi. Watu hao walikutwa na karatasi yenye ujumbe kwa aliyekuwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ulioandikwa: “Nasaha kwa Kova, mzee andaa kamati ya mazishi ya vipolisi vyako tukiwamaliza tutakufikia wewe.” Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema jana kuwa tukio hilo, lilitokea Jumamosi iliyopita, eneo la Fire, jijini Arusha wakati mtuhumiwa Athumani Kassim alipokamatwa eneo la Engosheraton akiwa na silaha na aliwataja wenzake. Kamanda Sabas alisema walipopata taarifa kutoka kwa raia wema walio tilia shaka mwenendo wa mtuhumiwa huyo ambaye alipokamatwa, alikutwa na milipuko, makoti makubwa mawili na kofia ya kuficha uso. “Baada ya mahojiano, alituambia kuna wenzake wawili anashirikiana nao kufanya uhalifu na tuliweka mtego. “Saa 5 usiku, askari wetu wakiwa wameambatana na Kassim, walipofika jirani ka

MBUNGE WA KAWE HALIMA MDEE ATUPWA RUMANDE

Image
  Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akiwasili katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na tuhuma za shambulio la mwili kwa Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam,  Theresia Mbando. M bunge huyo alinyimwa dhamana na kutupwa rumande. (Picha na Francis Dande) Halima Mdee (katikati) akiwa na mbunge wa Bunda, Ester Bulaya (wa pili kushoto) pamoja na wafuasi wa Chadema wakati akielekea mahabusu.    Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akisindikizwa na Ofisa wa Polisi, nyumba yake aliyeshika faili kuelekea mahabusu baada ya kunyimwa dhamana katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam. Mwanasheria wa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Prof. Abdallah Safari ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, baada ya mbunge huyo kunyimwa dhamana

POLISI WAZIMA MAANDAMANO YA WANAFUNZI WA KILICHOKUWA CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU JOSEPH TAWI LA SONGEA

Image
Mmoja wa vijana ambaye anasadikiwa ndiye aliyekuwa kinara wa kuhamasisha maandamano ya wanafunzi wa vyuo vya Mtakatifu Joseph vya Tawi la Songea vilivyofungwa na serikali  akiwa chini ya ulinzi wa kikosi cha kuzuia fujo FFU kutokana na kufanya maandamano kinyume cha utaratibu wakitaka kwenda kumuona Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi wakati walipodhibitiwa maeneo ya shule ya Bunge posta wakielekea wizarani leo. TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ilifuta kibali kilichoanzisha vyuo vikuu viwili vishiriki vya Mtakatifu Joseph ambavyo ni Chuo Kikuu kishiriki cha Sayansi ya Kilimo na Teknolojia (SJUCAST) na Chuo Kikuu kishiriki cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (SJUIT) vilivyopo Songea. (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) Baadhi ya askari wakijiandaa kuzuia maandamano ya wanafunzi hao leo maeneo ya wizara ya Fedha na Mipango Posta  jijini Dar es salaam. Wanafunzi hao wakifurumushwa na polisi mara baada ya kuktwa wakiandamana b

HARMONIZE AUFUNGA MWEZI WA PILI NA BADO KAMSHIRIKISHA DIAMOND PLATNUMZ.

Image
Dar es Salaam, Tanzania – February 29, 2016: Mwimbaji anaekuja kwa kasi kwenye muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva) kutoka Tanzania anayewakilisha kundi la Wasafi Classic Baby( Wcb ),Harmonize ameachia wimbo wake wimbo mpya unaoitwa ‘BADO’ aliyomshirikisha Diamond Platnumz. SABABU YA KUREKODI WIMBO HUU. Kwa singo mbili alizosikika Harmonize(Aiyola,Kidonda Changu) kwenye vyombo vya habari,jamii imekua ikimfananisha sana na Diamond kwenye uimbaji,ndipo siku moja Harmonize wakati akiimba Diamond alivutiwa na Melody ya wimbo huu na kusema hii itakua nafasi ya Watanzania kuwatofautisha kwenye uimbaji. KUHUSU WIMBO WA BADO. Harmonize alikaa na Diamond akamuuliza ni msichana gani alishamuumiza kiasi kwamba hawezi kumsahau,ingawa Diamond hakumwambia ni msichana gani,lakini akamwambia hiyo ni idea(Mwanga) mzuri wa kutunga wimbo ‘mkali’ Beat ya wimbo huu imetengenezwa na Mtayarishaji(Producer) anaitwa Fraga na kabla ya kurekodi kwenye studio ya Wasafi,producer Fraga alimtumi

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA MTWARA

Image
Waziri Mkuu, Kassim majliwa akitoa agizo la kusimamishwa kazi Daktari wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Fortunatus Namahala (kulia) baada ya kutajwa kuwa alidai rushwa ya sh.100, 000/= ili aweze kumtibu baba mzazi wa Tatu Abdallah (wapili kulia) wakati alipoitembelea hospitali hiyo Februari 29, 2016.  Wamawake wakiwa wametandika khanga kwenye wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Februari 29, 2016.Waziri Mkuu, Kassim majaliwa alitembelea wodi hiyo na kukemea mtindo huo akiwataka wauguzi na waganga kutandika mashuka yahospitali ambayo alisema ana taarifa kuwa yapo ili kuepusha hatari ya wananwake hao kubeba magonjwa kupitia kahanga hizo watokapo hospitalini hapo.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea hospitali ya Mkoa wa Mtwara Februari 29, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Halima Dendego na kulia Ni Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt.Shaibu Maarifa.  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waganga, Wauguzi na wafanyakazi wa Hosp