WAZIRI MKUU MAJALIWA ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA MTWARA
Waziri
Mkuu, Kassim majliwa akitoa agizo la kusimamishwa kazi Daktari wa
Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Fortunatus Namahala (kulia) baada ya
kutajwa kuwa alidai rushwa ya sh.100, 000/= ili aweze kumtibu baba mzazi
wa Tatu Abdallah (wapili kulia) wakati alipoitembelea hospitali hiyo
Februari 29, 2016.
Wamawake
wakiwa wametandika khanga kwenye wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mkoa wa
Mtwara, Februari 29, 2016.Waziri Mkuu, Kassim majaliwa alitembelea wodi
hiyo na kukemea mtindo huo akiwataka wauguzi na waganga kutandika
mashuka yahospitali ambayo alisema ana taarifa kuwa yapo ili kuepusha
hatari ya wananwake hao kubeba magonjwa kupitia kahanga hizo watokapo
hospitalini hapo.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea hospitali ya Mkoa wa Mtwara Februari
29, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Halima Dendego na kulia Ni
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt.Shaibu Maarifa.
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waganga, Wauguzi na wafanyakazi wa
Hospitali ya Mkoa wa Mtwara wakati alipoitembelea Februari 29, 2016.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa kujenga zahanati na nyumba ya
mganga kwenye kijiji cha Nandagala, wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Msaada
huo wenye thamani ya dola za Marekani 55,000 (sawa na sh. Milioni
119.35) umetolewa na kampuni ya Huawei Technologies yenye makao yake
jijini Dar es Salaam. Pia wametoa kompyuta za mezani (desktop) 25
pamoja na UPS 25 kwa ajili ya shule tano za sekondari wilayani humo.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo jana (Jumapili,
Februari 28, 2016) Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei, Bw. Bruce Zhang
alisema kampuni yake imetoa msaada huo ikiwa ni mwitikio wa sera ya
Wizara ya Afya inayotaka kila kijiji kiwe na zahanati na kila kata iwe
na kituo cha afya.
Wakati
huohuo, kampuni ya mtandao wa simu ya Halotel ilimkabidhi Waziri Mkuu
hundi ya sh. Milioni 9/- ambazo ni mchango wao wa kumsaidia Waziri Mkuu
ambaye pia ni mbungewa jimbo la Ruangwa ili zisaidie kulipia familia
zisizo na uwezo kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Akizungumza
na wanakijiji hao kabla ya kukabidhi hundi hiyo, Meneja Mkuu Msaidizi
wa Biashara wa Mkoa wa Lindi, Bw. Sebastian Innocent alisema: "Mchango
huu utazihusu kaya 900 ambazo zinalipiwa sh. 10,000 kila moja. Kila kaya
inatakiwa kulipia watu sita, hivyo tutaweza kuwafikia watu 5,400
kupitia mchango huu.
Alisema
kampuni yao imejenga minara 50 katika mkoa wa Lindi ambapo 40 inafanya
kazi na minara 22 kati ya 40 imeunganishwa na inatoa huduma ya 3G.
Akitoa
shukrani kwa misaada yote, Waziri Mkuu alisema anaishukuru kampuni ya
Halotel kwa kumsaidia kulipia sh. Milioni 9/- kwa ajili ya CHF ambazo
alisema zimegawanywa katika vijiji 90 vya wilaya nzima ya Ruangwa na kwa
kaya 10 za watu sita sita.
Aliwashukuru
kwa kuweka minara katika wilaya hiyo jambo ambalo alisema litasaidia
wananchi kupata mawasiliano ya simu kwa urahisi zaidi.
Kuhusu
zahanati, Waziri Mkuu Majaliwa aliishukuru kampuni ya Huawei
Technologies kwa msaada huo ambao alisema utakapokamilika, utawapunguzia
wananchi adha ya kwenda kijiji cha jirani kupata huduma ya matibabu.
Alisema
ana mpango wa kuweka nguvu ya umeme jua (solar power systems) kwenye
shule zote za msingi, shule zote za sekondari na zahanati zote kwenye
wilaya ya Ruangwa ambayo ndiyo jimbo lake ili asiwepo mtoto wa kushindwa
kusoma au mtu kupata matibabu kwa sababu ya kukosa umeme. Wilaya ya
Ruangwa ina shule za msingi 82, shule za sekondari 15, vituo vya afya
vitatu na zahanati 28.
Waziri Mkuu alirejea Mtwara jana hiyo hiyo na leo hii amerejea Jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Wauguzi na Madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara wakimsikiliza
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao hospitalini hapo
Februari 29, 2016. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akiagana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa
Mtwara, Shaibu Maarifa kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara kabla ya kurejea
Dar es slaam Februari 29, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim majaliwa akitazama ngoma kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara
kabla ya kuondoka kurejea Dar es salaam Februari 29, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Comments
Post a Comment