Mtoto wa Odinga amekiri kuwa alikosea alipodai kuwa bonde la Olduvai Gorge liko Kenya.
Mwanawe aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga, Rosemary, amekiri
kuwa alikosea alipodai kuwa bonde la Olduvai Gorge liko Kenya ilhali
liko Tanzania.
''Bonde la Oldupai ama Olduvai liko Tanzania, nimekubali kuwa nilikosea nilipokuwa nikihutubia mkutano wa viongozi wa vijana kutoka kote duniani nikiwa New York Marekani(International Young Leaders Assembly).
''Nahisi kama ambaye nimewakosea ndugu zangu kutoka Tanzania''. ''Nia yangu ilikuwa ni kusema kuwa nilipokuwa mdogo nikienda shuleni nilifunzwa kuwa fuvu la mtu wa kale lilipatikana Olorgesaiile eneo la Kajiado.

Nisemeje ,,nawaombeni radhi Watanzania. Olduvai Gorge iko salama wala
haijanyakuliwa na kenya 'Katika ile hali ya undugu naomba kuwanyoshea
mkono wa amani kwa sababu mwisho wa siku Afrika mashariki ndio kitovu
cha ubinadamu'' alisema bi Odinga kupitia mtandao wake wa Instagram.
Tamko lake kuhusiana na bonde hilo la Olduvai (Oldupai) lililoko
Tanzania lilihusiana na mada ya siku hiyo.
Olduvai ndiko kulikopatikana vifaa vilivyotumika na watangulizi wa binadamu yapata miaka milioni moja na laki sita iliyopita (milioni 1.6)
Olduvai ndiko kulikopatikana vifaa vilivyotumika na watangulizi wa binadamu yapata miaka milioni moja na laki sita iliyopita (milioni 1.6)
Bi Rosemary aliomba radhi baada ya kuzomewa na maelfu ya watu kwenye
mitandao ya kijamii ya Facebook Instagram na Twitter wakidai
aliwapotosha hadhira yake na haswa ulimwengu kwa kusema eti Olduvai ipo
Kenya.
Mbunge Zitto Kabwe alikuwa amechangia mada kwa kusema kuwa Tanzania
sharti izinadi vivutio vyake vya kitalii ilikuzima dhana potovu.
Aidha alidai kuwa watu wanafikiria kuwa mlima kilimanjaro uko Kenya
ilahali ukweli halisi upo Tanzania sawa na mwanamuziki nyota Diamond
Platnumz ambaye ni Mtanzania
Comments
Post a Comment