NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI, KATIBU MKUU WALA VIAPO KUIONGOZA TUME YA UTUMISHI YA JESHI LA POLISI NA MAGEREZA
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akila kiapo cha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akila kiapo cha kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) akimpongeza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masau...