Ndege Yapotea ikiwa na watu 23
Ndege ndogo ya shirika la ndege la tara Airlines iliyokuwa na watu 23 wakiwemo watoto imepota ikiwa maeneo ya usawa wa milima Magharibi mwa Nepal.
Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka
Pokhara, Magharibi mwa Mji Mkuu Kathmandu, kwenda Jomsom, eneo ambalo
watu wengi wanaoenda kukwea milima ya Himalaya huanza safari yao ya
kukwea milima hiyo.
Ripoti zinasema mabaki ya ndege hiyo yamepatikana ingawa hakuna taarifa zozote kuhusu vifo au majeruhi.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, Ndege hiyo
ilipoteza mawasiliano na maafisa wa udhibiti wa safari za ndege wa
Pokhara dakika 18 baada ya kupaa na kwamba hakuna viwanja vya ndege kati
ya maeneo hayo mawili.
Maafisa wanasema ndege hiyo ya shirika
la Tara Airlines ilikuwa na marubani watatu na abiria 20, mmoja wao raia
wa China na mwingine wa Kuwait. Wawili kati ya abiria waliokuwa
wamebebwa na ndege hiyo walikuwa watoto.
Tangu mwaka 1949, kumetokea zaidi ya ajali 70 zilizohusisha ndege za kawaida na helikopta, na vifo vya watu 700.
Comments
Post a Comment