NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI, KATIBU MKUU WALA VIAPO KUIONGOZA TUME YA UTUMISHI YA JESHI LA POLISI NA MAGEREZA
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akila kiapo cha
kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na
Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto)
jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi
kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu,
Ilvin Mugeta. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
akila kiapo cha kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na
Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto)
jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi
kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu,
Ilvin Mugeta. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) akimpongeza Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni mara baada ya
kumuapisha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi
na Magereza, katika tukio lililofanyika katika Mahakama hiyo, jijini
Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa
askari Polisi na Magereza.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapa kuwa Katibu wa Tume
ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa
Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo
inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza.
Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) akimkaribisha ofisini
kwake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni
kabla ya kumuapisha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi
la Polisi na Magereza, katika tukio lililofanyika katika Mahakama hiyo,
jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi
kwa askari Polisi na Magereza.. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kushoto),
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia)
wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, mara
baada ya Jaji huyo kuwaapisha kuwa viongozi wa Tume ya Utumishi ya Jeshi
la Polisi na Magereza katika tukio lililofanyika Mahakamani hapo,
jijini Dar es Salaam leo. Injinia Masauni katika Tume hiyo amekuwa
Makamu Mwenyekiti, na Meja Jenerali Rwegasira amekuwa Katibu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Comments
Post a Comment