Posts

MILIPUKO YA MABOMU YAUWA WATU ZAIDI YA 7A INDONESIA

Image
Jengo la mgahawa wa Starbucks Coffee lililopo Mji Mkuu wa Indonesia, Jakarta ambapo mabomu hayo yamelipuliwa mapema leo. Milipuko ya mabomu takribani sita imetokea katika Mji Mkuu wa Indonesia, Jakarta na baadaye ufyatulianaji mkali wa risasi na watu zaidi ya saba wameripotiwa kuuawa japo polisi wanasema huenda kuna idadi kubwa zaidi ya waliouawa. Kati ya hao waliouawa ni maofisa watatu wa polisi, raia wawili akiwemo Mreno mmoja pamoja na washambuliaji watano. Polisi wa Indonesia wakijihami Milipuko imetokea maeneo kadha, ikiwa ni pamoja na mgahawani katika duka la kibiashara lililoko karibu na Ikulu ya rais wa nchio hiyo na ofisi za Umoja wa Mataifa (UN). Kuna ripoti za maafisa wa polisi kuonekana kwenye majengo na barabara za mji huo karibu na kituo hicho cha kibiashara. Eneo hilo limezingirwa na maafisa wa usalama. Rais Joko Widodo amehimiza raia wawe na utulivu na kushutumu “kitendo hicho cha ugaidi”. “Tunaomboleza watu waliofariki kwa sababu ya kisa h...

MISS TANZANIA APEWA TALAKA KISA SOMA HAPA

Image
Miss Tanzania 2011, Salha Israel. IMELDA MTEMA, AMANI Ndoa ya Miss Tanzania 2011, Salha Israel aliyofunga na Abdulatif Fundikira ‘Tiff’ ambaye ni mtalaka wa mwanamitindo Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ aliyeko gerezani kwa msala wa madawa ya kulevya huko Macau, China, inasemekana kuingia mdudu mbaya baada ya mrembo huyo kudaiwa kupewa talaka moja. Kwa mujibu wa chanzo makini, kumekuwa na kutoelewana kati ya wanandoa hao, jambo ambalo limewafanya kuwa kwenye sintofahamu kila wakati huku wakimsaka mchawi wa ndoa yao. Salha Israel akiwa na mumewe. “Awali wale watu walikuwa wanapendana sana lakini cha ajabu kumekuwa na migogoro midogomidogo kwenye ndoa yao hadi kufikia wakati wenyewe wanajiuliza mchawi ni nani ilihali wao wanaonekana wanapendana sana,” kilisema chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa wanandoa hao. Baada ya ishu hiyo kutua kwenye dawati la gazeti hili, mwanahabari wetu alianza kwa kumsaka Tiff ambaye a...

Mastaa Hawa na Mchezo Huu Vepeee?

Image
Wema Sepetu na Aunt Ezekiel Miongoni mwa mastaa wa filamu na muziki Bongo wamekuwa na viashiria vya vitendo visivyofaa hasa wanapokuwa kwenye sehemu za starehe na wengi wao ni wale wanaotumia kinywaji chenye kilevi. Wanaotajwa sana kwenye tabia hiyo mni pamoja na hawan wafuatao kutokana na picha zao kuzagaa nsana mitandaoni na kwenye magazetin mbalimbali. Hapa nawazungumzia Aunt Ezekiel na Wema Sepetu, Isabela Mpanda na Baby Madaha, Rayuu na Skaina nk. Mastaa hawa kwa nyakati tofauti wamekuwa wakionesha wazi viashiria hivyo kwa kupigana picha na picha hizo kuzagaa kwenye vyombo vya habari. Wao kwao imekuwa kama fasheni na muda mwingi hulichukulia suala hili kama la kawaida kwa madai kuwa ni kutokana na ukaribu wa urafiki walionao. Skaina na Rayuu Je, kabla ya ustaa walikuwa wakisalimiana na kuwa karibu hivi? Ni swali ambalo linaulizwa na kila msomaji pengine na hata wazazi wanaowazunguka kwani kwao ni vitu vigeni. Ustaa ndiyo shinikizo la viashiriahivi...

Miss Tanzania ataka namba ya Samatta

Image
Mshiriki wa Miss Tanzania 2005 ambaye pia ni mcheza fi lamu, Maureen Gislary. Imelda Mtema,Dar es Salaam MSHIRIKI wa Miss Tanzania 2005 ambaye pia ni mcheza fi lamu, Maureen Gislary ameibuka na kutaka namba ya simu ya mchezaji wa timu ya Taifa Stars na Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, Mbwana Samatta kwa gharama yoyote. Mbwana Samatta. Akizungumza na Amani Sports, Maureen aliyekuwa kumi bora katika kinyang’anyiro hicho cha Miss Tanzania kilichoshuhudiwa kwa Nancy Sumari kuibuka mshindi alisema kuwa, nia ya kuhitaji namba hiyo nikuhakikisha anamuweka Samatta ‘kibindoni’ kabla hajatimkia nje ya nchi. “Kwanza nimefurahishwa sana na ushindi wake wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani mwaka 2015, mwenye namba yake tafadhalini naiomba kwa gharama yoyote nitatoa,” alisema Maureen.

TANZANIA ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA RWANDA-MAJALIWA.

Image
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura. Ambapo amemuahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Rwanda. Akizungumza na Balozi Kayihura jana ,(Jumatano 13, 2016) ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu amemshukuru Balozi huyo kwa kumtembelea na ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendeleza ushirikiano ulipo baina ya nchi hizi mbili. “Nia yetu ni kushirikiana kwa pamoja kwa kuunganisha wafanyabiashara wetu, kwa kutumia Bandari ya Dar es salaam na reli ya kati, ambayo tutajenga kwa kiwango cha kisasa ‘standard gauge’ ili ziweze kubeba mizigo mingi na kwenda mwendo wa kasi” alisema Waziri Mkuu. Kwa upande wake, Balozi wa Rwanda, Kayihura amesema Tanzania na Rwanda ni nchi marafiki na zinafanyakazi wa pamoja, Rwanda iko tayari kushirikiana na Tanzania kikanda na kimataifa. “Tunatumia Bandari ya Dar es salaam na Mombasa, tunashukuru kwa namna ambavyo mnaboresha Bandari ya Dar e...

SPIKA WA BUNGE AENDA KUMFARIJI MAMA MARIA NYERERE

Image
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiweka saini kitabu cha maombolezo  alipokwenda kutoa pole Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa kufiwa na mkwewe Leticia Nyerere leo tarehe 13 Januari Msasani jijini Dar es Salaam. Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimfariji Bi. Rose Nyerere binti wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alipokwenda kuwafariji kufuatia kuondokewa na Mpedwa wao Leticia Nyerere. Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsalimia Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alipokwenda nyumbani kwake kumpa pole kufuatia kifo cha mkwewe wake Leticia Nyerere. Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsikiliza Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere (aliyekaa katikati) wakati alipokwenda kumpa pole kufuatia kifo cha mkwewe wake Leticia Nyerere. Aliyekaa kulia ni Mmoja wa Wasemaji wafamilia Bw. John Shibuda. Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na  Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa Mwalim...