MILIPUKO YA MABOMU YAUWA WATU ZAIDI YA 7A INDONESIA
Jengo la mgahawa wa Starbucks Coffee lililopo Mji Mkuu wa Indonesia, Jakarta ambapo mabomu hayo yamelipuliwa mapema leo.
Milipuko ya mabomu takribani sita imetokea katika Mji Mkuu wa Indonesia, Jakarta na baadaye ufyatulianaji mkali wa risasi na watu zaidi ya saba wameripotiwa kuuawa japo polisi wanasema huenda kuna idadi kubwa zaidi ya waliouawa.
Kati ya hao waliouawa ni maofisa watatu wa polisi, raia wawili akiwemo Mreno mmoja pamoja na washambuliaji watano.
Polisi wa Indonesia wakijihami
Milipuko imetokea maeneo kadha, ikiwa ni pamoja na mgahawani katika duka la kibiashara lililoko karibu na Ikulu ya rais wa nchio hiyo na ofisi za Umoja wa Mataifa (UN).
Kuna ripoti za maafisa wa polisi kuonekana kwenye majengo na barabara za mji huo karibu na kituo hicho cha kibiashara.
Eneo hilo limezingirwa na maafisa wa usalama.
Rais Joko Widodo amehimiza raia wawe na utulivu na kushutumu “kitendo hicho cha ugaidi”.
“Tunaomboleza watu waliofariki kwa sababu ya kisa hiki, lakini pia tunakilaani. Kimevuruga utulivu na amani na kuingiza wasiwasi miongoni mwa raia,” amesema.
Msemaji wa polisi, Anton Charliyan ameambia wanahabari kuwa maafisa wa polisi na raia ni miongoni mwa waliofariki.
Bado haijabainika ni nani huenda amehusika katika shambulio hilo.
Indonesia, taifa lenye Waislamu wengi zaidi duniani, imeshambuliwa na makundi ya wapiganaji wa Kiislamu awali.
Majuzi, imekuwa kwenye hali ya juu ya tahadhari kutokana na tishio kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State.
Hili ndilo shambulio la kwanza kubwa kutokea Jakarta tangu mashambulio kwenye hoteli za Marriot na Ritz mwaka 2009.
Hali ilivyokuwa baada ya tukio hilo Eneo ambapo moja ya bomu limelipuliwa. Hali ya taharuki wakati mabomu yakiripuka Polisi wakifanya juhudi za kupambana na taharuki hiyo …Miili ya waliouawa Polisi akiimarisha ulinzi Miili ya waliouawa ikifunikwa Jeshi la Usalama la Indonesia wakipambana na walipuaji wa mabomu hayo Kikosi chaJeshi la Usalama la Indonesia wakiwa katika hekaheka ya kupambana na adha hiyo.
Majeruhi wakipewa msaada. Mmoja wa ofisa wa polisi aliyejeruhiwa kwa bomu akiokolewa. Anayedhaniwa kuwa mtuhumiwa akiwanyooshea bastola raia Polisi wakizidi kuimarisha ulinzi. Eneo la tukio. Polisi akijihami.Anayedhaniwa kuwa mmoja wa watuhumiwa akikatiza na bunduki mkononi. Ofisa wa Polisi akiamurisha kikosi chake kupambana na walipuaji.Mbwa wa polisi akipelekwa eneo la tukio ili kufanya utafiti wa kubaini walipuaji wa mabomu hayo.
Polisi wakichukua tahadhari.
PICHA NA DAILY MAIL
Comments
Post a Comment