Posts

Wema atumbua Mil.300

Image
Wema Sepetu ‘Madam’. Na Mwandishi Wetu WEMA Sepetu ‘Madam’ ni mashine ya kutafuna fedha! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia habari za mjini kumtaja staa huyo wa Bongo Movies kuwa ameteketeza takriban Sh. Mil. 300 za mbunge ambaye anadaiwa kuwa ndiye anayemweka mjini kwa sasa, Risasi Mchanganyiko limenasa ubuyu kamili. KUMBUKUMBU MUHIMU Wema na mbunge huyo (jina kapuni kwa sasa) wanadaiwa kuwa walianzisha uhusiano wa kimapenzi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana ambao matokeo yake yalimpa ushindi Dk. John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Inadaiwa uhusiano huo tayari umezaa matunda kwani mlimbwende huyo ni mjamzito. TUJIUNGE NA CHANZO Kwa mujibu wa chanzo makini, mara baada ya mrembo huyo asiyechuja Bongo kuwa ‘klozi’ na mbunge huyo kijana mwenye pesa ndefu katika kampeni hadi sasa, amemchuna mbunge huyo kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya matumizi na zawadi mbalimbali ali

TRA YAVUKA LENGO YAKUSANYA TRILIONI 1.4 KWA MWEZI

Image
  kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) (Katikati) Alphayo Kidata akisisitiza jambo wakati alipofanya mazungumzo na waandishi wa habari kuhusu taarifa za ukusanyaji wa mapato wa kila mwezi Kushoto ni Kaimu Kamishna wa Forodha Jocktan Kyamuhanga na kulia    ni Kaimu Kamishna wa Kodi za Ndani Yusufu Salum .   Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) (Katikati) Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa za ukusanyaji wa mapato wa kila mwezi. Picha Na raymond Mushumbusi MAELEZO   Jumla ya shilingi trilioni 1.4 imekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi cha mwezi Desemba mwaka uliopita wa 2015. Kiasi hicho ni sawa na ongezeko la wastani wa shilingi  bilioni 490 kwa mwezi ukulinganisha na wastani wa makusanyo ya kuanzia Julai hadi Novemba ambapo ,TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi bilioni 900 kwa mwezi. Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Kamishna Mamlaka ya Mapato

BREAKING NEWZZ: MOTO WA WA RAIS MAGUFULI SASA KILA KONA WAWAKA WATUMISHI 9 WAMETIMULIWA KAZI LEO

Image
Watumishi 9 wakiwemo wakuu wa idara 7 wasimamishwa kazi kwa kuuza majengo ya serikali na kuisababishia hasara ya Sh milioni 9 Kigoma CHANZO: RADIO ONE

Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira afanya ziara makao makuu ya Vodacom Tanzania‏

Image
Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira,Mhe Anthony Mavunde (wapili toka kushoto) akikagua vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini vya mfanyakazi wa kigeni wa Vodacom Tanzania , Valentino Giron (kushoto),wakati alipofanya ziara ya kikazi Makoa makuu ya Vodacom Tanzania yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam hivi karibuni,Anayeshuhudia kulia ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu. Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira,Mhe Anthony Mavunde(Kulia) akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,wakati alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam hivi karibuni kwa ajili ya kujua kero na maendeleo mbalimbali ya wafanyakazi wa kampuni hiyo. Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira,Mhe Anthony Mavunde(Mwenye suti katikati)akimsikiliza Mkuu wa kitengo cha rasilimali watu wa Vodacom Tanzania, Conrad Msoma (kushoto) wakati alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam hivi karibuni kwa ajili

BREAKING NEWS : KIMENUKA IRINGA ASUBUHI,VIONGOZI WATUMBULIWA KWA UFISADI

Image
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mwigulu Nchemba amewasimamisha kazi viongozi wa vyama vya msingi vya tumbaku mkoani Iringa wanaotuhumiwa kushiriki katika ufisadi wa mkopo wa matrekta tisa kupitia mgongo wa vyama vya msingi vya wakulima wa tumbaku na kujimilikisha wenyewe. Nchemba alifikia hatua hiyo jana baada ya wakulima wa tumbaku kulalamikia viongozi wa vyama hivyo na kuwataka wakabidhi ofisi. Awali, mwanachama wa Chama cha Msingi cha Mfyome, Francis Kilatu alisema Benki ya CRDB inawakata fedha zao huku wamiliki wa matrekta hayo wakiwa ni wengine hivyo alimuomba waziri kulishughulikia mara moja.

BREAKING NEWS : WAZIRI MKUU AWATUMBUA VIONGOZI WENGINE RUVUMA,MOTO WAWAKA KILA KONA

Image
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kusindika tumbaku cha mkoani Ruvuma na kuwasimamisha kazi viongozi wa  Chama Cha Kikuu Cha Ushirika cha SONAMCU. Akizungumza jana jioni(Jumanne, Januari 5, 2016), katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu Ndogo ya Songea, wakati alipokutana na wakulima wa zao la tumbaku wa Wilaya ya Namtumbo, Wananchama wa Vyama Vya Ushirika vya Mkoa wa Ruvuma, viongozi wa Mkoa pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini. Waziri Mkuu amesema, Serikali ina dhamira ya kufufua kiwanda cha kusindika tumbaku cha SONAMCU, na lengo la kutembelea kiwanda hicho ni katika utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli la kufufua viwanda nchini. Waziri Mkuu Majaliwa, ametembelea maeneno mbalimbali ya kiwanda hicho na kukagua mitambo iliyokua ikitumika kusindika tumbaku, kabla kiwanda hicho kuzimwa miaka kadhaa iliyopita baada ya kukosa malighafi za kuend

Rais Obama Adondosha Chozi Hadharani Akitetea Hoja

Image
Rais Barack Obama akitokwa. Rais Barack Obama alitokwa na machozi jana alipokuwa akitetea kufanyiwa mabadiliko kwa sheria za udhibiti wa silaha nchini Marekani ili kupunguza idadi ya watu wanaoshambuliwa na kuuawa kwa risasi nchini humo. Obama aliwaambia Wamarekani kwamba mageuzi anayoyatete  ni kwa manufaa yao wenyewe kwa kuwa yeye huu ni mwaka wake wa mwisho kukaa madarakani na wala hana mpango wa kugombea tena. Rais Obama anataka watu wote wanaouza silaha washurutishwe kuwapekua na kuchunguza historia ya watu wanaowauzia silaha. Kwa sasa, sheria hiyo hugusa tu wauzaji silaha waliosajiliwa. Wauza silaha ambao hawajasajiliwa, hutakiwa kuwauliza tu wateja wao iwapo wamewahi kupatikana na makosa ya uhalifu au kama wana matatizo ya kiakili. Hatua hiyo ya Rais Obama imepingwa vikali na baadhi ya viongozi wakuu wa chama cha Republican wanaosema inaingilia uhuru wa kikatiba wa Wamarekani.

Aliyepongeza majambazi yaliyovamia Polisi Stakishari… ahukumiwa jela

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Bruno Kimaryo, kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kusambaza ujumbe katika mtandao wa kijamii wa kuyapongeza majambazi yaliyovamia Kituo cha Polisi cha Stakishari na kuua polisi.  Aidha, mshtakiwa huyo ametakiwa ama kulipa faini ya Sh. 600,000 kwa kosa hilo. Katika tukio la Stakishari lililotokea Julai 12, mwaka huu, majambazi yalivamia kituo hicho na kuua polisi wanne na raia watatu pamoja na kupora bunduki 20 aina ya Sub Machine Gun (SMG). Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mkuu, Waliarwande Lema, baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi watano wa upande wa mashtaka. Alisema vielelezo vitano na utetezi wa mshtakiwa vinaonyesha kuwa Bruno alifurahia kitendo kilichofanywa na majambazi hao na alitamani kila kituo cha polisi kivamiwe. Alisema mshtakiwa huyo katika ujumbe wake huo alitumia viunganishi vya maneno yasiyokuwa ya kibinadamu ya auawe, avamiwe na kuwa utetezi wake unaungana na

BREAKING NEWZZ:MTUHUMIWA WA MAUAJI ARUSHA AKAMATWA

Image

Rais Magufuli amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya RAHCO

Image
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO) Mhandisi Benhadard Tito (kulia). Rais wa Jamhuri ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO) Mhandisi Benhadard Tito ili kupisha uchunguzi wa kina kufuatia ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi uliobainika katika mchakato wa utoaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema, Rais Magufuli amefikia uamuzi huo baada ya kuitisha kikao cha wataalamu kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za serikali ambazo zinahusika katika utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani “Standard Gauge” Amesema pamoja na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO, Rais Magufuli ameivunja bodi ya RAHCO baada ya kujiridhisha kuwa haikutekeleza ipasavyo wajibu wake katika kusimamia mchakato wa zabuni hiyo na badala

KIMENUKA..Wema Sepetu Atimuliwa Kwenye Nyumba..Aliyodai Kainunua Kwa Sh Million 280

Image
Mizigo ikipakizwa kutoka kwenye nyumba hiyo. Musa Mateja UFALME umeanguka! Unaweza kusema hivyo! Hatimaye Miss Tanzania 2006, aliye pia staa wa filamu za Bongo, Wema Isaac Sepetu amedaiwa kutimuliwa kwenye nyumba ambayo alipanga kwa mbwembwe na kualika waandishi wa habari ili watoe ‘nyuzi’ hewani, akidai ni yake kwa kuinunua kwa shilingi milioni 280, fuatana na Ijumaa Wikienda. Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Wema amekumbwa na kadhia hiyo ya kuhamishwa kwenye nyumba hiyo iliyopo Makumbusho jijini Dar, usiku wa Desemba 18, mwaka huu. SIKIA CHANZO “Jamani mmesikia kilichomtokea Wema Sepetu? Yaani huyu dada anaishi kwa maigizo hadi basi. Lile sakata lake la kudaiwa kutumia umeme na maji kimagumashi limemtokea puani, maana kwenye umeme pekee yake nasikia anadaiwa zaidi ya shilingi milioni nane (8,000,000) fedha ambazo imekuwa shida kulipa.” Mizigo ikiwa kwenye gari. BABA MWENYE NYUMBA AINGIA KATI “Sasa baba mwenye nyumba ameingilia kati. Ameamua kulipa ye

CCM yanyakua ubunge jimbo la Masasi

Image
Mbunge Mteule wa Jimbo la Masasi kwa tiketi ya CCM, Bw. Rashid Chuachua. Chama cha Mapinduzi kimeweza kutetea jimbo lake la Masasi katika uchaguzi ulifanyika jana baada ya kuahirishwa Okt. 25 mwaka huu kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia chama cha NLD, Dkt. Emamanuel Makaidi kufariki Dunia huko Nyangao mkoani Lindi. Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi huo yaliyotangazwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya jimbo la Masasi, Fortunatus Kagoro amesema kuwa Bw. Rashid Chuachua amepata kura 16,597 akifuatiwa na Ismail Makombe maarufu kama Kundambanda wa CUF, aliyepata kura 14,019. Wengine walioshiriki katika uchaguzi huo ni Swaleh Ahmad wa CHADEMA, aliyepata kura 512, Omary Timothy wa ACT-Wazalendo aliyepata kura 347, na Angelus Thomas wa NLD aliepata kura 70. Wakati huo huo katika harakati za Uchaguizi wa Ubunge katika jimbo la Ludewa Wafuasi watatu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Jimbo la Ludewa wameshambuliwa na watu wanao daiwa kuwa ni w

Rais Magufuli Akutana na Maalim Seif Ikulu leo Kuongelea Mgogoro wa Uchaguzi wa Zanzibar

Image
Rais Magufuli amekutana na kuzungumza na mgombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif juu ya mgogoro wa uchaguzi wa Zanzibar TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Nora adaiwa kuwa chizi tena!

Image
Mwigizaji wa kitambo Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’. Na Brighton Masalu NURU Nassoro ‘Nora’ ambaye ni mwigizaji wa kitambo Bongo,anadaiwa kuugua uchizi kwa mara nyingine tena, jambo ambalo amelipinga vikali na kwamba wabaya wake wameendelea kumtakia mabaya katika maisha yake, lakini yuko safi na anaendelea na maisha yake. Mwanzoni mwa wiki hii, mmoja wa rafiki zake wa karibu aliliambia gazeti hili kuwa, uzushi na uvumi huo ulianza kuenezwa wiki mbili zilizopita, hali iliyosababisha watu wengi, kuanza kumtumia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS),wakitaka kuthibitisha uvumi huo, hali iliyomuumiza msanii huyo. Baada ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Nora kupitia simu yake ya mkononi ambapo alikiri kukumbwa kukutana na madai hayo huku akionesha masikitiko makubwa juu ya uvumi huo. “Mwenyewe nilishangaa sana, nilishindwa kujua ni kwa nini watu wanaendelea kunitakia mabaya kiasi hiki, nilianza kupokea simu kutoka kwa watu wangu wa karibu wakiniuliza kulikoni, lakini mbay

Dkt. Kingwangalla asiamama getini kudhibiti watumishi wachelewaji Wizara ya Afya

Image
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akisimamia zoezi la ufungwaji wa geti hilo, Kulia ni askari wa SUMA JKT akiweka kufuli katika lango kuu la kuingia katika ofisi za Wizara ya Afya. Dkt Kingwangalla akiwauliza askari wa getini kuhusu daftari la mahudhurio ya watumishi wa wizara baada ya kufungwa geti hilo, na kupewa maelezo kuwa watumishi huonyesha vitambulisho pekee na husaini katika vitengo vyao. Mmoja wa wafanyakazi wa Wizara ya Afya akiwasili ofisini huku muda wa kuingia kazini ukiwa umepitiliza. Kushoto ni Naibu Waziri, Dkt Kingwangalla akizungumza na mmoja watumishi wa wizara hiyo na kuagiza kuletewa vitabu vya mahudhurio kwa vitengo vyote vilivyopo wizarani hapo. Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara ya Afya, Michael John akitoa maelezo kuhusu mahudhurio ya watumishi kwa Dkt Kingwangalla. Magari ya watumishi wa Wizara ya Afya yakiendelea kuwasili ofisini bila ya kutambua kuwa Mheshimiwa Dkt Kigwangalla

MAN ARRESTED, QUESTIONED AFTER SH 720M CASH FOUND IN HIS HOTEL ROOM

Image
There was drama at a hotel in Dodoma after TSh 720 million was found in the room of a middle-aged man. The mid-morning incident fuelled speculation that CCM nomination candidates were splashing billions of shillings. The Citizen could not, however, independently verify that the money found at the hotel was in any way related to the ongoing political campaigns, especially the high-stakes process to nominate CCM’s presidential candidate. The development took place as CCM was holding meetings to pick its flag-bearer. Rival camps in the party immediately pointed an accusing finger at one another over the huge stash of money found in possession of the Indian national. Supporters of the various camps used social media to speculate on who may have been behind the matter, with most linking it with an alleged plot to bribe members of the CCM National Congress, which was due to convene last night. Mr Bernard Membe, who was in the short list of five candidates picked by the Central Committ

BREAKING NEWS : BOT

Image

BREAKING NEWZZ.....RAIS MAGUFULI AWASIMAMISHA KAZI VIGOGO 4 WALIO SAFIRI KWENDA NJE YA NCHI

Image
Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi wanne wa Takururu ambao walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma. Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi. Bw Sefue amesema atakayekiuka agizo la rais "atachukuliwa hatua kali”. Hii si mara ya kwanza kwa Dkt Magufuli kuwachukulia hatua maafisa wa Serikali tangu achukue madaraka mwezi uliopita. Siku chache baada ya kuingia afisini, a libadilisha usimamizi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili baada ya kufanya ziara ya kushtukiza huko na kutoridhishwa na utoaji huduma

Lowassa kufanya ziara nchi nzima kuanzia kesho

Image
Edward Lowassa. Aliyekuwa mgombea urais wa Chadema akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa ataanza ziara ya kuzunguka nchi nzima kuwashukuru Watanzania kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 na kesho atakuwa Tanga. Katika ziara hiyo, Lowassa ataambatana na viongozi waandamizi wa Chadema na Ukawa kuwashukuru wananchi kwa namna walivyounga mkono upinzani na ajenda nzima ya mabadiliko katika Uchaguzi Mkuu uliopita. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene imesema kiongozi huyo atatoa shukrani zake kwa wananchi kwa jinsi wanavyoendelea kuweka matumaini yao kwa upinzani. Taarifa hiyo ilieleza kwamba wananchi bado wanaamini kwamba upinzani ndiyo nguzo imara wanayoitegemea katika kuwaletea mabadiliko ya kweli kwa ajili ya maendeleo yao na ustawi wa Taifa kwa ujumla. “Wananchi wanastahili shukrani kwa imani hiyo kubwa ambayo ni ishara