Wema atumbua Mil.300


WEMAMAWema Sepetu ‘Madam’.
Na Mwandishi Wetu
WEMA Sepetu ‘Madam’ ni mashine ya kutafuna fedha! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia habari za mjini kumtaja staa huyo wa Bongo Movies kuwa ameteketeza takriban Sh. Mil. 300 za mbunge ambaye anadaiwa kuwa ndiye anayemweka mjini kwa sasa, Risasi Mchanganyiko limenasa ubuyu kamili.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Wema na mbunge huyo (jina kapuni kwa sasa) wanadaiwa kuwa walianzisha uhusiano wa kimapenzi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana ambao matokeo yake yalimpa ushindi Dk. John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Inadaiwa uhusiano huo tayari umezaa matunda kwani mlimbwende huyo ni mjamzito.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, mara baada ya mrembo huyo asiyechuja Bongo kuwa ‘klozi’ na mbunge huyo kijana mwenye pesa ndefu katika kampeni hadi sasa, amemchuna mbunge huyo kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya matumizi na zawadi mbalimbali alizomnunulia.
WEMA37
Gari la Wema aina ya Range Rover Evoque.
RANGE MIL 200
“Mbunge alimpa ahadi tu akimaliza kampeni anampa zawadi ya Range Rover yenye thamani ya shilingi milioni 200, ilikuwa maalum kwa ajili ya bethidei yake maana hakuweza kufanya sherehe hiyo iliyomuangukia akiwa kwenye kampeni. Alipomaliza tu, mtoto wa kike akapewa ndinga yake japo alificha kwa kusema amejizawadia mwenyewe.
SHOPPING USIPIME!
“Yaani Wema akiwa ndani ya kampeni alikuwa halali hoteli za kimaskini, hizo shopping ndiyo usiseme. Kipindi kile cha kampeni shopping moja tu ya viatu, cheni, gauni na mazagazaga mengine ilikuwa si chini ya milioni mbili au tatu hivi. Kafanya nyingi tu za aina hiyo.
“Sasa achana na hizo, kwenye sherehe za Krismasi, Boxing Day na Mwaka Mpya nasikia katekeketeza milioni 25 kwa mavazi na mazagamazaga aliyopika kula yeye na marafiki zake wa karibu pamoja na ndugu zake, mbunge kasimamia shoo bila wasiwasi wowote,” kilisema chanzo hicho.
KUKAA HOTELI DAR
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, baada ya kumaliza kampeni, Wema alirejea jijini Dar lakini kutokana na hali yake alimwambia mbunge amlipie hoteli kwani hakujisikia kuendelea kuishi pale Kijitonyama alipokuwa anaishi.
wema-11
Nyumba mpya anayoishi Wema.
ATEKETEZA MIL. 40
“Yaani huwezi amini pale hotelini (jina lipo) aliteketeza kitu kama shilingi milioni 40 hivi kwa kupanga na kula kwa zaidi ya siku 15. Mbunge hapo alikunjuka tu bila wasi maana fedha kwake si tatizo.
NYUMBA MIL. 12
“Baada ya kuona mmiliki wa nyumba ya Kijitonyama amemtaka Wema kuhama katika nyumba yake, kigogo akaona isiwe tabu, akampangia nyumba nyingine kali zaidi maeneo ya Ununio jijini Dar kwa shilingi milioni 12 kwa mwaka mzima.
MISELE YA MAFUTA, STAREHE MIL. 23
“Wema muoneni hivihivi tu, mtu wake anayemsimamia kaniambia kwa kuweka mafuta kwenye gari, tangu mwezi wa 11 mwaka jana alipoanza kulitumia lile Range, kateketeza shilingi milioni na kama haitoshi, ametumia shilingi milioni 13 kwa ajili ya mitoko ya usiku kuwapa watu watunze na yeye kutunza wanamuziki mbalimbali katika bendi ukijumlisha na vinywaji na vyakula,” kiliweka nukta chanzo hicho.
wema-21NI REKODI YA AINA YAKE
Akizungumzia matumizi hayo ya fedha, mmoja wa mastaa wakubwa ambaye aliomba hifadhi ya jina, alisema kwa matumizi hayo makubwa aliyoyafanya Wema ndani ya miezi kadhaa ni dhahiri kwamba ndiye staa wa kwanza wa kike kutumia fedha nyingi ndani ya muda mfupi.
“Wewe fikiria tunasikia kina Lulu, Kajala na wengineo wamepangiwa nyumba lakini husikii kama kuna gharama nyingine kubwa kama Range, mafuta, shopping, kupanga hoteli ambazo kwa ujumla wake zinafikia shilingi milioni 300,” alisema staa huyo.
MBUNGE ASAKWA
Jitihada za kumpata mbunge huyo machachari aliyekuwa akitema cheche mara kwa mara kwa viongozi wa vyama vya upinzani, hazikuzaa matunda lakini rafiki yake wa karibu alikiri kuwa mbunge huyo amemwaga fedha nyingi kwa Wema.
“Daah jamaa (mbunge) kafa kaoza hizo milioni 300 mbona kidogo ni zaidi ya hizo, wewe unafikiri tangu kipindi cha kampeni hadi leo na matumizi ya Wema yanayohusisha na wapambe wake ni mchezo?” alisema rafiki huyo.
WEMA ANASEMAJE?
Alipotafutwa Wema ili kuzungumzia matanuzi hayo simu yake iliita bila kupokelewa licha ya kutumiwa ujumbe mfupi, bado hakujibu.

Comments

Popular posts from this blog