Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira afanya ziara makao makuu ya Vodacom Tanzania
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira,Mhe Anthony Mavunde (wapili toka kushoto) akikagua vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini vya mfanyakazi wa kigeni wa Vodacom Tanzania , Valentino Giron (kushoto),wakati alipofanya ziara ya kikazi Makoa makuu ya Vodacom Tanzania yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam hivi karibuni,Anayeshuhudia kulia ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu.
Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira,Mhe Anthony Mavunde(Kulia) akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,wakati alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam hivi karibuni kwa ajili ya kujua kero na maendeleo mbalimbali ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira,Mhe Anthony Mavunde(Mwenye suti katikati)akimsikiliza Mkuu wa kitengo cha rasilimali watu wa Vodacom Tanzania, Conrad Msoma (kushoto) wakati alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam hivi karibuni kwa ajili ya kujua kero na maendeleo mbalimbali ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment