Rais Obama Adondosha Chozi Hadharani Akitetea Hoja

ObamaRais Barack Obama akitokwa.
Rais Barack Obama alitokwa na machozi jana alipokuwa akitetea kufanyiwa mabadiliko kwa sheria za udhibiti wa silaha nchini Marekani ili kupunguza idadi ya watu wanaoshambuliwa na kuuawa kwa risasi nchini humo.
Obama aliwaambia Wamarekani kwamba mageuzi anayoyatete  ni kwa manufaa yao wenyewe kwa kuwa yeye huu ni mwaka wake wa mwisho kukaa madarakani na wala hana mpango wa kugombea tena.
Rais Obama anataka watu wote wanaouza silaha washurutishwe kuwapekua na kuchunguza historia ya watu wanaowauzia silaha. Kwa sasa, sheria hiyo hugusa tu wauzaji silaha waliosajiliwa. Wauza silaha ambao hawajasajiliwa, hutakiwa kuwauliza tu wateja wao iwapo wamewahi kupatikana na makosa ya uhalifu au kama wana matatizo ya kiakili.
Hatua hiyo ya Rais Obama imepingwa vikali na baadhi ya viongozi wakuu wa chama cha Republican wanaosema inaingilia uhuru wa kikatiba wa Wamarekani.

Comments

Popular posts from this blog