BREAKING NEWS : KIMENUKA IRINGA ASUBUHI,VIONGOZI WATUMBULIWA KWA UFISADI


Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mwigulu Nchemba amewasimamisha kazi viongozi wa vyama vya msingi vya tumbaku mkoani Iringa wanaotuhumiwa kushiriki katika ufisadi wa mkopo wa matrekta tisa kupitia mgongo wa vyama vya msingi vya wakulima wa tumbaku na kujimilikisha wenyewe.
Nchemba alifikia hatua hiyo jana baada ya wakulima wa tumbaku kulalamikia viongozi wa vyama hivyo na kuwataka wakabidhi ofisi.
Awali, mwanachama wa Chama cha Msingi cha Mfyome, Francis Kilatu alisema Benki ya CRDB inawakata fedha zao huku wamiliki wa matrekta hayo wakiwa ni wengine hivyo alimuomba waziri kulishughulikia mara moja.

Comments

Popular posts from this blog