BREAKING NEWZZ.....RAIS MAGUFULI AWASIMAMISHA KAZI VIGOGO 4 WALIO SAFIRI KWENDA NJE YA NCHI



Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi wanne wa Takururu ambao walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma.
Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi.
Bw Sefue amesema atakayekiuka agizo la rais "atachukuliwa hatua kali”.
Hii si mara ya kwanza kwa Dkt Magufuli kuwachukulia hatua maafisa wa Serikali tangu achukue madaraka mwezi uliopita. Siku chache baada ya kuingia afisini, a libadilisha usimamizi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili baada ya kufanya ziara ya kushtukiza huko na kutoridhishwa na utoaji huduma

Comments

Popular posts from this blog