Posts

Mitikisiko ya Pwani yaitikisa Dar Live

Image
Mwibaji wa kundi la Excellent (katikati)akiselebuka na wanenguaji wake. Hadija Kopa nae akionyesha umahili wake wa kuimba na kucheza. Wanamuziki wa Ogopa Kopa taarabu wakiserebuka. Ma Mc wa onyesho hilo Mc pilipili na Dida wakipozi kupigwa picha. Nyota Waziri akicheza na shabiki wake.   Nyota Waziri akimpagawisha shabiki kwa sauti tamu. Msagasumu akiwarusha mashabiki. Mzee yusufu nae akikonga nyoyo za mashabiki waliofika kwenye onyesho hilo. Wanenguaji wa kibao kata wakifanya yao. Jana usiku ndani ya ukumbi wa Taifa wa burudani wa Dar Live kulikuwa na onyesho la Mitikisiko ya Pwani onyesho hilo lilizikutanisha bendi mbalimbali za taarabu za hapa jijini Dar es Salaam. Bendi hizo ni Jahazi, Excellent, Ogopa kopa na Wakali wao, pia kulikuwa na vikundi vya Baikoko, Kibao kata na Msagasumu aidha mwanadada Nyota Waziri pia alitoa burudani katika onyesho hilo.

Masogange kumzalia Davido?

Image
  Video Queen anayekimbiza Bongo, Agness Masogange. HUENDA ikawa kweli Video Queen anayekimbiza Bongo, Agness Masogange amenasa ujauzito unaosemekana kuwa ni wa staa wa muziki kutoka Naija, Davido baada ya kuweka picha tata mtandaoni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Masogange aliweka picha ya Davido na kuandika ‘I’m missing him’ na baada ya sekunde kadhaa tena akaweka picha nyingine ilioonesha majibu ya ujauzito kuwa amenasa. Hata hivyo baada ya kuandamwa na mashabiki alizifuta zote hali iliowafanya mashabiki wawe njia panda.Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza Novemba mwaka huu katika sherehe ya kuzaliwa ya Davido. Kama kweli Masogange atakuwa na ujauzito kama inavyosemakana na ikajulikana ni wa Davido basi Davido atakuwa na mtoto wa pili baada ya wa kwanza aliyenaye ambaye amezaa na Sophie Momodu wa Nigeria. (Imetayarishwa na Andrew Carlos/Gpl)

Mwanamke wa kwanza achaguliwa Saudi Arabia

Image
Mmoja wa wanawake Saudi Arabia akipiga kura. Wananchi wa Saudi Arabia wameweka historia kwa kumchagua mwanamke wa kwanza kuwa mwakilishi wao katika uchaguzi uliofanyika jana. Tume ya uchaguzi ya Saudia Arabia imetangaza. Salma bint Hizab al-Oteibi alichaguliwa kuwa mwanamke wa kwanza mwakilishi wa wilaya katika Jimbo la Mecca. Wanawake Saudi Arabia wakitoka kupiga kura kuwachagua viongozi wao. Japo matokeo ya uchaguzi huu yanaendelea kutangazwa tangazo hilo limeibua hisia miongoni mwa wenyeji. Hii ndio iliyokuwa mara ya kwanza wanawake kupiga kura na kushiriki kama washindani. Maofisa wa Serikali walisema kuwa wanawake 130,000 walijiandikisha kupiga kura, ambayo ni moja ya kumi ya wapiga kura wanaume. Kuna zaidi ya wagombea 1,000 wanaong’ang’ania viti mbalimbali katika huo. Wanawake hawa walikuwa wakifanya kampeni zao huku wamesimama nyuma ya pazia au wakati mwingine wanawakilishwa na mwanaume. Wanawake kadhaa wa Saudi Arabia wamepongeza uchaguzi huo kama hatua muhim

WAKATI WAPINZANI WAKIPINGA UTEUZI WA WAZIRI PROFESA MUHONGO MWENYEWE ATOA KAULI NZITO AFUNGUKA KILA KITU

Image
WAKATI wapinzani wakipinga uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, waziri huyo amewasihi wananchi kumvumilia kidogo, ili baada ya muda mfupi atoe mpango wa maendeleo ya wizara hiyo, ambao pamoja na mambo mengine, utaelezea bei ya nishati hiyo itakavyoshuka.  Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, Profesa Muhongo alisema mbali na mkakati wa kushusha bei ya umeme, kasi ya kusambaza umeme vijijini kupitia miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), itarejea palepale. “Nimepokea uteuzi huo, kinachofuata ni kuwatumikia wananchi, niwaombe tu wanivumilie kidogo nitawapa mpango wangu wa maendeleo wa muda mfupi na mrefu, lakini nisisitize tu nishati sio siasa, ni suala la utaalamu, liachwe lifanywe kitaalamu,” alisema Profesa Muhongo. Akizungumzia bei ya umeme na upatikanaji wake, Profesa Muhongo alisema kupunguza bei hiyo ni ajenda muhimu itakayozingatiwa na kusema il

BREAKING NEWS:WAZIRI WA KWANZA KUTIMULIWA NA RAIS MAGUFULI HUYU HAPA

Image
Rais John Magufuli alionya Mawaziri aliowataja juzi kuwa tayari kufanya sherehe ya kufukuzwa, kama pia wataandaa sherehe za kuteuliwa kushika nyadhifa hizo katika Baraza la kwanza la serikali yake ya awamu ya tano. Katika kauli yake hiyo mbele ya waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema anataraji Mawaziri aliowachagua wawe wachapa kazi, wenye lengo la kuleta maendeleo nchini kwa kasi. Akitangaza Baraza lake hilo ikiwa ni siku ya 35 tangu aapishwe kuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, Rais Magufuli alisema: “Na kwa hakika, wasihangaike kufanya sherehe. Wamepata kazi ngumu, wakafanye kazi, lakini kama wapo ambao wanaopenda kufanya sherehe, pia wajiandae kufanya sherehe siku wakifukuzwa. “’Contract’ (mkataba) yetu ni miaka mitano, tukawafanyie Watanzania yale tuliyoyaahidi, bila kubagua rangi, dini, itikadi, ukanda, makabila, ndiyo maana siku zote nimekuwa nikisema Hapa ni Kazi Tu.” Lakini si lazima Waziri adumu kwa miaka mitano ya

KAMPUNI YA AZAM YAMDINDIA MAGUFULI,NI KUHUSU AGIZO LA SIKU SABA,TRA YAWAANGUKIA WATANZANIA,SOMA HAPO KUJUA

Image
Kaimu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Dk. Philip Mpango akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) juu ya hatua za ulipaji wa kodi iliyokwepwa katoka katika kontena 329 katika bandari Kavu ya Azam,leo jijini Dar es Salaam. Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii KAMPUNI 15 zimeshindwa kulipa kodi za kontena zilizotoroshwa katika bandari kavu ya Azam inayomilikiwa na Said Salim Bakhressa na kodi iliyokuwa imekwepwa kwa kampuni 43 ni zaidi ya Sh. Bilioni 12.      Kodi iliyolipwa ya Kontena 329 hadi jana ambayo ndio ilikuwa ulipaji wa hiari kwa ndani ya siku saba za Rais Dk. John Pombe Magufuli ni zaidi ya sh. bilioni 10 pekee.       Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamisha Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Dk. Philip Mpango amesema kuwa kampuni hizo zinatakiwa kulipa kodi hiyo kwani ulipaji wa hiari wa siku saba za Rais Dk. John Pombe Magufuli umeisha jana  hivyo hatua zitachukuliwa kuh

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii na Jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri , leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Katiba na Sheria, Harrison Mwakyembe katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Ashantu Kijaji katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri, leo katika ukum

BREAKING NEWZZZZ!! KILICHOJIRI MAHAKAMA KUU KANDA YA SHINYANGA LEO,JAMES LEMBELI APENYA KIZINGITI CHA KWANZA

Image
Kushoto ni aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Kahama Mjini James Lembeli (Chadema) akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Juma Protas wakitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga leo asubuhi baada ya kushinda maombi yao ya kuomba kupunguziwa gharama za kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi uliompa ushindi Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini,Jumanne Kishimba ambapo Lembeli alipaswa kulipa shilingi milioni 15 na badala yake Mahakama imemtaka kulipa Shilingi milioni 9 ndipo kesi ya msingi ianze kusikilizwa-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog Lembeli akitoka Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga akiwa na uso wa furaha baada kuvuka kiunzi cha kwanza katika kesi namba 1 ya mwaka 2015 aliyofungua Novemba 23,mwaka huu kupinga matokeo yaliyompa ushindi mgombea wa CCM,Jumanne Kishimba,katika uchaguzi mkuu uliopita nchini Tanzania Baada ya kufungua kesi hiyo James Lembeli

WATUHUMIWA 40 WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA UKWEPAJI KODI.

Image
Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akionyesha picha ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES LTD,ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini ambaye anatuhumiwa kwa kutoa makontena 329 kwenye bandari kavu ya AZAM (AZAM ICD) bila kulipia kodi anayetafutwa na jeshi hilo pia ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni za “JAS EXPRESS FREIGHT LTD” na “XL CLEARING AND FOWARDING Co. LTD” ambazo zote zilitumika kutoa makontena hayo. Ameonyesha picha ya mtuhumiwa huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 40 ambao wanahojiwa kwa tuhuma za kula njama na kuikosesha serikali mapato. Uchunguzi unafanywa kwa pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kubaini jinsi ambavyo makontena 329 na mengine 2489 yalivyotolewa bandarini kinyume cha taratibu. Kati ya hao, watuhumiwa 26 ni watumishi w

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 08.12.2015

Image
       N,

MUHUMBILI YAPATIWA MSAADA WA MASHINE YA KISASA YA DIGITAL YA X-RAY

Image
Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu matumizi ya mashine mpya ya X-ray ya digitali.  Dk Lwakatare amesema mashine hiyo ina uwezo wa kupiga picha na kutumwa nje ya nchi kwa ajili ya ushauri wa kitaalamu zaidi. Mashine hiyo haihitaji chumba cha kusafishia picha wala dawa za kusafishia. Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akitoa maelezo kuhusu idadi ya wagonjwa waliopata huduma ya kipimo cha CT Scan baada ya mashine hiyo kukamilika. Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne ikipokelewa leo  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne ikipokelewa leo  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). ……………………………………………………………………………… Hospitali ya Taifa  Muhimbili (MNH) imepata mashine mpya na ya kisasa ya Digital X-ray ambayo wataalamu wake hawatalazimika kutu