WATUHUMIWA 40 WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA UKWEPAJI KODI.
Kati
ya hao, watuhumiwa 26 ni watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA)na watumishi 03 kutoka Bandari kavu (ICD) YA AZAM wanatuhumiwa
kuhusika na upotevu wa makontena 329. Aidha, watuhumiwa 11 ambao ni
watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa kuhusika na upotevu
wa makontena 2489.
Uchunguzi unaoendelea pia unahusisha kupitia kumbukumbu mbalimbali na kadhia za forodha ili kubaini mtindo uliotumika na kuwabaini wote waliohusika katika mchakato huo. Makontena 329 yaligundulika kukosekana kwenye ICD ya AZAM kuanzia mwezi Julai hadi Novemba 2015, wakati makontena 2489 yaligundulika kutolewa Bandarini kuanzia Mwezi Machi mpaka Septemba, Mwaka 2014 kinyume cha taratibu kwa lengo la kukwepa kodi na ushuru.
Uchunguzi bado unaendelea ili kuwabaini wote wanaohusika na hatimaye majalada ya kesi yatapelekwa kwa mwanasheria wa serikali ili watuhumiwa watakaobainika kuhusika na makosa mbalimbali wafikishwe mahakamani.

Kamanda
wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akizungumza na waandishi
wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na watuhumiwa 40
washikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum kwa tuhuma za ukwepaji
kulipa kodi pamoja na mtu mmoja ambaye anatafutwa na Jeshi la Polisi
ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES
LTD,ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini.
Meneja
wa Huduma na elimu kwa mlipa kodi kutoka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania,
Diana Masalla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
leo kuhusiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kukusanya jumla ya
shilingi 10,075,979,462.08 kutoka kwa makampuni 22 ambayo yalihusika na
uondoshwaji wa makontena bandarini kinyume cha sheria na taratibu za
forodha hadi kufikia tarehe 10 Desemba 2015.
Pia
kati ya hao makampuni 06 amesema kuwa yamelipa kodi yote iliyokadiriwa
pamoja na adhabu, ambapo makampuni 16 yamelipa sehemu ya kodi
iliyokadiriwa pamoja na adhabu.
Aidha, makampuni 26 hayajalipa kodi kiasi cha shilingi 4,789,924,609.69 pamoja na kwamba zoezi la ukadiriaji limefanyika.
hata
hivyo amesema kuwa leo ni siku ya mwisho iliyotolewa na Mheshimiwa Rais
kwa wafanyabiashara waliokwepakulipa kodi ya makontena,
Amewasisitiza
wananchi wote watoe taarifa kuhusu vitendo vya ukwepaji kodi kutumia
namba 0784210209. Pia taarifa za mwenendo wa wafanyakazi wa TRA Wasio
waadilifu zitolewe kupitia simu namba 0689 122515 na ujumbe mfupi 0689
122516.
Baadhi
ya Waandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano na Kamanda wa Kanda
Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova wakimsikiliza leo jijini Dar es
Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
Comments
Post a Comment