BREAKING NEWZZZZ!! KILICHOJIRI MAHAKAMA KUU KANDA YA SHINYANGA LEO,JAMES LEMBELI APENYA KIZINGITI CHA KWANZA
Kushoto ni aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Kahama Mjini James Lembeli
(Chadema) akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Juma Protas wakitoka katika
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga leo asubuhi baada ya
kushinda maombi yao ya kuomba kupunguziwa gharama za kesi ya kupinga
matokeo ya Uchaguzi uliompa ushindi Mbunge wa Jimbo la Kahama
Mjini,Jumanne Kishimba ambapo Lembeli alipaswa kulipa shilingi milioni
15 na badala yake Mahakama imemtaka kulipa Shilingi milioni 9 ndipo kesi
ya msingi ianze kusikilizwa-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Lembeli akitoka Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga akiwa na uso
wa furaha baada kuvuka kiunzi cha kwanza katika kesi namba 1 ya mwaka
2015 aliyofungua Novemba 23,mwaka huu kupinga matokeo yaliyompa ushindi
mgombea wa CCM,Jumanne Kishimba,katika uchaguzi mkuu uliopita nchini
Tanzania
Baada ya kufungua kesi hiyo James Lembeli alipaswa kulipa gharama za
kesi kiasi shilingi kisichozidi milioni 15,kwa washtakiwa watatu ambao
ni Jumanne Kishimba,Msimamizi wa Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali.Hata hivyo James Lembeli akiongozwa na Wakili Joachim Hamis
kutoka Kampuni ya Mpoki and Associates Advocate aliwasilisha maombi
katika Mahakama hiyo akiomba kupunguziwa gharama hiyo kwa mujibu wa
sheria.
Muonekano wa jengo la Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga.
Maombi hayo yalipingwa na Mawakili watatu wa upande serikali Solomon
Lwenge na Muyengi Muyengi wakiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali,Pendo
Makondo,wakidai kiasi hicho Lembeli anaweza kukilipa kwa kuwa amekaa
miaka 10 katika nafasi ya ubunge.
Kulia ni aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Kahama Mjini James Lembeli
(Chadema) akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Juma Protas wakitoka katika
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga wakitoka mahakamani.
Akisoma hukumu ya maombi hayo,Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya
Shinyanga,Victoria Makani,amesema kuwa mbunge kwa muda wa miaka kumi
hakuna mahusiano na gharama ya kesi hivyo aliridhishwa na maombi ya
Lembeli ya kufikiriwa kupunguziwa gharama hiyo na kumtaka alipe shilingi
milioni 9 badala ya 15 ndani ya siku 14 ndipo kesi ya msingi ipangwe
kuanza kusikilizwa.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Kahama
mkoani Shinyanga Juma Protas akizungumza na waandishi wa habari baada
ya kutoka mahakamani
Lembeli akiwa na uso wa furaha mahakamani,ambapo tayari amelipa shilingi milioni 9 ili kesi ya msingi ianze kusikilizwa.
Mheshimiwa James Lembeli akizungumza na waandishi wa habari mahakamani
ambapo ameishukuru mahakama hiyo kwa kutenda haki kwake katika maombi
yake aliyowasilisha akidai kiwango cha awali kilikuwa kikubwa-Picha zote
na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Comments
Post a Comment