MAAJABU MAKUBWA DAR! MTOTO AZALIWA BILA UBONGO WA NYUMA!
Mtoto anayedaiwa kuzaliwa bila ya ubongo wa nyuma(medulla oblongata).Na Haruni Sachawa NI maajabu! Mwanamke mmoja, Diana Dioniz mkazi wa Magomeni Makuti jijini Dar es Salaam, ameangua kilio cha kuomba msaada baada ya mtoto wake aliyezaliwa mwaka mmoja uliopita kugundulika kuwa hana ubongo wa nyuma (medulla oblongata), hali inayosababisha shingo kulegea na macho kutoona. Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake, Diana alisema alipata ujauzito wa mtoto huyo na kujikuta akiwa na furaha kubwa, lakini baada ya kuzaliwa na kumpa jina la John, amejikuta akipata mateso makubwa, kwani kwa muda wote, shingo yake inakuwa imelegea na macho yake hayaoni. “Majirani walinishauri nimpeleke hospitali kwa uangalizi zaidi, nilipomfikisha Muhimbili nikaambiwa suala la mwanangu linapaswa kushughulikiwa na daktari bingwa wa magonjwa ya watoto wa Kitengo cha Moi,” alisema mwanamke huyo. Aliongeza kuwa, baada ya kupelekwa huko na kuchunguzwa ndipo ilipojulikana kuwa na matatizo hayo, ambay